MIRADI 47 YA MAENDELEO KUTEMBELEWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KILIMANJARO

MOSHI-KILIMANJARO.

MWENGE wa Uhuru mwaka wa 2026 unatarajiwa kupitia miradi ya maendeleo 47 yenye jumla ya thamani ya Bilioni 52, 556,284,070.02 mkoani Kilimanjaro.

Hayo yameelezwa Juni 22,2026 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu wakati akitoa taarifa za ujio wa Mwenge huo wa Uhuru mkoani humo kwa waandishi wa habari.

Alisema mkoa huo unatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru mkoani Kilimanjaro ukitokea Mkoa wa Tanga Juni 28, mwaka huu, katika kata ya Hedaru iliyoko Wilaya ya Same na kukimbizwa katika halmashauri zote saba zilizoko katika Wilaya sita za Mkoa huo.

Alisema kuwa wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru, jumla ya miradi 24 itawekewa mawe ya msingi, miradi 17, itazinduliwa na miradi 6 itakaguliwa.

Alisema kuwa miradi yote hiyo ya mkoani Kilimanjaro imezingatia Kauli mbiu za Mbio za Mwenge mwaka 2026 inayosema TANZANIA NI YETU SOTE,TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KULETA MAENDELEO "

Aidha Babua alisema miradi hiyo imegusa sekta zote muhimu za kimaendeleo ambazo ni pamoja na elimu miradi 7, afya miradi 7, maji miradi sita, barabara na madaraja miradi 6, miradi ya uwekezaji binafsi miradi 7 na miradi ya kijamii saba.

Alisema mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu, zinatarajiwa kukamilika Julai 4, wilayani Siha na kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Arusha Julai 5, mwaka huu, katika uwanja wa shule ya sekondari Tingatinga iliyoko wilaya ya Longido.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.