RC BABU; USHIRIKIANO WA VIONGOZI NI MSINGI WA MAENDELEO KILIMANJARO

MOSHI-KIKIMANJARO.

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya viongozi wa kisiasa na watumishi wa umma ni msingi muhimu wa kuleta maendeleo kwa wananchi. 

Alitoa kauli hiyo Machi 19,2026, wakati wa hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Priscus Tarimo mjini Moshi.

Babu alieleza kuwa kukaa pamoja na kuzungumza kama viongozi na wananchi husaidia kufikia malengo ya maendeleo na kuimarisha mshikamano wa jamii.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava, alisifu hafla hiyo kwa kuwakutanisha watu wa dini mbalimbali, akisema ni njia nzuri ya kuimarisha umoja.

Akiwakilisha Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shaaban Mlewa aliitaka serikali kulinda maadili wakati wa sikukuu za kidini kama Eid El-Fitri.

Naye Tarimo alieleza kuwa Iftar hiyo ni sehemu ya sadaka ya mwezi wa Ramadhani, yenye lengo la kukuza upendo, mshikamano na umoja miongoni mwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.