UWT MOSHI KUTEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA SAMARIA KUADHIMISHA MIAKA 49 YA CCM


Mwenyekiti wa UWT  Wilaya ya Moshi Ruwaichi Jacob Kaale, akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo kilichoketi Januari 24,2026.

MOSHI-KILIMANJARO.

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Wilaya ya Moshi, imepanga kutembelea kituo cha watoto yatima na wenye mahitaji maalum cha Samaria kilichopo katika Kata ya Uru Kusini, Wilaya ya Moshi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) yanayofanyika Februari 5 kila mwaka.

Hayo yamebainishwa Januari 24,2026 Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo, Ruwaich Kaale, wakati akifungua kikao cha kawaida cha Kamati ya Utekelezaji ya UWT Wilaya ya Moshi kilichofanyika katika Ofisi za CCM Wilayani humo.

Ruwaichi alisema jumuiya hiyo itafanya ziara hiyo Januari 27, 2026, kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali na jamii katika kuwasaidia watoto yatima na wenye mahitaji maalum kwa kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali ya kibinadamu kama sehemu ya kuadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM.

Kwa upande wake, Katibu wa UWT Wilaya ya Moshi, Oliver Ngalawa, alisema kikao hicho kililenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mikakati na mipango ya utekelezaji wa shughuli za jumuiya hiyo kwa kipindi kijacho.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.