SIMBA; URAIS HAUPATIKANI KWA NJIA YA MAANDAMANO


MOSHI-KILIMANJAO.

Meneja wa Kampeni wa Wilaya ya Moshi Mjini, Adam Best Simba, amesema hakuna nafasi ya kupata urais kwa njia ya maandamano, akisisitiza kuwa uchaguzi ndio njia halali ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi.

Amesema hayo Oktoba 22, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Ostabay, mtaa wa Kigongoni, kata ya Shirimatunda, wakati akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ibrahim Shayo, pamoja na mgombea udiwani wa kata hiyo.Francis Shio.

Akizungumza katika mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini, Faraji Swai, Katibu Mwenezi Athuman Mfuchu, viongozi mbalimbali wa chama pamoja na wananchi, Simba alieleza kuwa:

"Rais Samia Suluhu Hassan alichukua nafasi ya urais mwaka 2021 baada ya mtangulizi wake, Hayati John Pombe Magufuli, kufariki dunia, alikuja na ajenda ya 4R kwa ajili ya kusaka maridhiano kutoka kwa wapinzani ambao baadhi yao wakiwa wamekimbilia nje ya nchi.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan, alitafuta maridhiano kwa sababu Tanzania ni nchi ya amani, ustahimilivu, mageuzi, na ujenzi mpya."

Aidha, aliongeza kuwa: "Hawa wanaosema wanataka kuandamana, hakuna urais wa maandamano."

Simba ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa , aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kwenda kupiga kura kwa amani, akisisitiza kuwa usalama umeimarishwa vya kutosha kuhakikisha kila mtu anashiriki bila hofu.

"Tunawaomba wananchi wote wa Moshi Mjini, na hususan wa Kata ya Shirimatunda, wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kidemokrasia, siyo maandamano."













Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.