MWALIMU ALIYEMFUNDISHA IBRAHIM SHAYO, AMUOMBEA KURA

MIEMBENI-MOSHI.

"Ninamkumbuka sana Ibrahim Shayo nikiwa mwalimu wake alipokuwa mwanafunzi katika shule ya msingi, alikuwa kijana mwenye nidhamu, mchapa kazi, mwenye maono na bidii ya kufanikisha malengo yake.

Leo hii ninajivunia kumuona akigombea Ubunge wa Jimbo la Moshi kama mwalimu wake wa zamani, namuombea kura kwa moyo wote.

Naamini atawawakilisha wananchi wa jimbo la Moshi mjini kwa uadilifu, ufanisi na kwa dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo. 

Wapiga kura wa Jimbo la Moshi mjink, tafadhali mpeni nafasi mwanafunzi huyu wangu, Ibrahim Shayo aonyeshe nia yake njema kwa vitendo katika kuwatumikia.”

Mwl. Verynace Monyo.















Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.