MGOMBEA UDIWANI KATA YA SOWETO AAHIDI KUPIGANIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

MOSHI-KILIMANJARO.

Mgombea udiwani wa Kata ya Soweto kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Maile, ameahidi kupigania ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo ili kuwapunguzia wananchi changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya.

Akizungumza Oktoba 19, 2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la Stendi za Bajaj Kata ya Soweto, Maile alisema kuwa kwa sasa kata hiyo haina kituo cha afya cha serikali na inategemea zahanati moja ndogo isiyo na miundombinu bora ya kutoa huduma za afya.

"Kata ya Soweto inahitaji kuwa na kituo cha afya kama kata nyingine, zahanati tuliyonayo ni ndogo na haina mazingira mazuri ya kutoa huduma bora, tukishirikiana na Mbunge, tutakwenda kujenga hoja ili kuishawishi serikali iweze kujenga kituo cha afya cha kisasa hapa Soweto,” alisema Maile.


Aliongeza kuwa kutokana na ukosefu huo, kina mama wajawazito, watoto na wazee hulazimika kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya St. Joseph inayomilikiwa na taasisi ya dini, jambo linaloongeza gharama na usumbufu kwa wananchi.

“Wananchi wa Soweto wanastahili kuwa na kituo cha afya cha serikali ndani ya kata yao, nikipewa ridhaa ya kuwa diwani wenu, nitapambana kuhakikisha ndoto hiyo inatimia,” aliongeza.


Mbali na sekta ya afya, Maile pia ameweka kipaumbele kwenye maendeleo ya michezo, akisema atashirikiana na wadau kuibua vipaji na kuunda timu ya kata yenye uwezo wa kushiriki ligi ya mkoa na hata ligi kuu.

“Tutashirikiana kuijenga Soweto yenye timu imara ya mpira wa miguu na michezo mingine. Vijana wetu wakipewa nafasi watafika mbali,” alisema.


Katika eneo la uwezeshaji wananchi kiuchumi, mgombea huyo ameahidi kuhakikisha fursa za mikopo na miradi ya maendeleo zinawafikia wananchi wote kwa usawa, bila upendeleo, ambapo, nitahakikisha kila mwananchi wa kata ya Soweto ananufaika na fursa hiyo.
















Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.