MAMA MZAZI WA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI IBRAHIM SHAYO, AMUOMBEA KURA RAIS SAMIA

MOSHI-KILIMANJARO.

Mama mzazi wa mgombea ubunge wa Jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ibrahim Shayo, na mgombea udiwani wa Kata ya Mjimpya, Abuu Shayo, Mariam Elikilia Shao, amewaomba wakazi wa Kata ya Mjimpya na Watanzania kwa ujumla kumpigia kura Rais Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Mariam alitoa kauli hiyo alipata fursa ya kuwasalimia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Oktoba 12, 2025 katika mtaa wa Sokoni, uliopo ndani ya Kata ya Mjimpya.

Akizungumza kwa hisia kali za kizalendo na uzalendo wa chama, alisema Rais Samia anapaswa kupewa ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi kutokana na kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.

“Yeyote mwana CCM wa kweli anaamini kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anastahili kuendelea kupewa dhamana ya kuliongoza taifa smeonyesha uwezo mkubwa, amesimamia maendeleo na kutoa fursa kwa wanawake kuonesha uwezo wao katika uongozi,” alisema Mariam.

Alieleza kuwa akiwa mzazi wa watoto wawili wanaowania nafasi tofauti za uongozi kwa tiketi ya CCM, anatambua thamani ya amani na utulivu, hivyo akatoa wito kwa wananchi kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, upendo na mshikamano.

Aidha, alisifu hatua ya Rais Samia kuimarisha hali ya uchumi na kuweka msukumo mpya kwenye utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, akisema hatua hiyo imeibua fursa nyingi kwa makundi hayo nchini.

"Mimi ni mwana CCM, natamani kumuona Rais Samia akiendelea tena, pia nawaomba wananchi wawachague wagombea wa CCM katika nafasi zote ili kuendeleza kasi ya maendeleo iliyoanzishwa,” alisisitiza.

Kauli hiyo ya mama wa wagombea imepokelewa kwa hisia chanya na wananchi waliohudhuria mkutano huo, wengi wakisema ni mfano wa kuigwa kwa wazazi wanaounga mkono siasa za maendeleo na uongozi wa kidemokrasia.

Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba 29, 2025, huku kampeni zikiendelea kufanyika kwa amani katika maeneo mbalimbali ya nchi.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.