BARREH AAGEUKIA MICHEZO, KUANZISHA MASHINDANO YA “BARREH CUP”

PASUA – MOSHI

Mgombea Udiwani wa Kata ya Pasua kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Barreh Farrah, ameahidi kuipa kipaumbele sekta ya michezo ikiwa atachaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Mtaa wa Relin,, Barreh alisema anapanga kuanzisha mashindano ya “BARREH CUP” yatakayoshirikisha vijana wa maeneo yote ya Kata ya Pasua.

"Michezo ni afya, ajira na njia ya kuwajenga vijana kimaadi, nitahakikisha kila kijana anapata nafasi ya kushiriki mchezo anaoupenda,” alisema Barreh mbele ya mamia ya wakazi wa eneo hilo.

Mbali na mashindano hayo, Barreh alieleza kuwa atawawezesha wanamichezo kwa kuwapatia mipira na jezi, huku akiahidi kushirikianaa na mbunge, kuimarisha miundombinu ya michezo ikiwemo viwanja vya wazi.

Tutaanza na BARREH CUP, lakini pia tutahakikisha relini na mitaa mingine inakuwa na timu imara,nia yangu ni kuona michezo inarudi katika hadhi yake,” aliongeza.

Barreh pia aliahidi kufufua michezo ya asili ikiwemo Rede na Mateka, ambayo zamani ilichezwa na wanawake lakini kwa sasa imeanza kusahaulika

Kwa upande mwingine, mgombea huyo aligusia pia sekta ya sanaa, akisema kuwa ataunga mkono wasanii wa filamu na muziki walioko ndani ya kata hiyo kwa kuwasaidia kukuza vipaji vyao.

"Tuna vijana wengi wenye vipaji vya sanaa, tukiwawezesha wanaweza kufika mbali, nitahakikisha wanapata nafasi ya kujieleza na kufanya kazi kwa uhuru,” alisema.

Barreh; ameweka msisitizo katika kuikuza sekta ya michezo na sanaa kama njia ya kuinua uchumi na ustawi wa vijana wa Kata ya Pasua.









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.