MGOMBEA UBUNGE CCM MOSHI MJINI AAHIDI MIKOPO NAFUU KWA VIJANA, USAWA KATIKA MGAO WA YA HALMASHAURI

MIEMBENI-MOSHI.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Moshi mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ibrahim Mohamed Shayo (IBRA-LINE) ameahidi kuhakikisha kuwa mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani ya halmashauri inawafikia walengwa wote bila ubaguzi endapo atachaguliwa kuwa mbunge.

Shayo aliyasema hayo Septemba 10,2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Miembeni, Manispaa ya Moshi mkoani humo na kuahidi kuwa mikopo hiyo itasimamiwa kwa uwazi ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi hasa vijana, wanawake na makundi maalum.

Pia alisema endapo atapata ridhaa ya kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Moshi mjini, atawawezesha waendesha bodaboda na bajaji kupata vyombo vya usafiri kwa mikopo isiyo na riba, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuwawezesha vijana kiuchumi na kupunguza ukosefu wa ajira.

Shayo pia aliahidi kuwa mesema kuwa mikopo hiyo itasimamiwa kwa uwazi ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi hasa vijana, wanawake na makundi maalum.

"Usimamizi bora wa fedha hizo ni nyenzo muhimu ya kuwakwamua wananchi kiuchumi na kuinua pato la kaya."alisema.

Katika hotuba hiyo, Shayo hakusita kuwaomba wananchi kumpigia kura Rais Samia Suluhu Hassan, akimuelezea kama kiongozi mahiri anayeleta mageuzi ya kweli, pamoja na kumuombea kura Haruna Mushi, mgombea udiwani wa kata hiyo.











Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.