CCM YAJIPANGA KUSHINDA KWA KISHINDO WILAYA YA MOSHI VIJIJINI

KINDI-MOSHI.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Vijijini kinajivunia kuwa na wanachama hai wapatao 95,000, hali inayokipa matumaini makubwa ya ushindi mnono katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na wanachama wa CCM katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Moshi Vijijini uliofanyika Septemba 12, 2025 katika Kata ya Kindi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Sirili Mushi, alisema chama hicho kina uhakika wa kupata kura nyingi kutokana na idadi kubwa ya wanachama waliopo.

“Wilaya ya Moshi Vijijini tunao wanachama hai 95,000, tunategemea kura zote hizo za chama chetu tuwe nazo, halafu nyingine tuongezee hadi kufikia kura 150,000,” alisema Mushi huku akihimiza wanachama kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi.

Aidha, alitumia jukwaa hilo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kuwachagua wagombea wa CCM, wakiwemo mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk.Samia Suluhu Hassan, mgombea mwenza Dk. Emanuel Nchimbi, pamoja na Wabunge na Madiwani wa chama hicho.

“Hakuna sababu ya CCM kushindwa kwa sababu mtaji wetu tunao sisi wenyewe,” alisisitiza Mushi.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.