Kauli Mbiu: "Tujenge Rau Mpya kwa Mshikamano Na Maendeleo ya Kweli".
Stallone Hamis Malinda, mgombea udiwani wa Kata ya Rau kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), amewashukuru Wajumbe wa mkutano mkuu wa kata hiyo kwa kumuamini na kumpatia ushindi wa kura 89, akiwapiku wagombea wengine William Gasper Kiwia aliyepata kura 16 na Sergius Andrea Mwise aliyepata kura 4.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Malinda aliwaahidi wananchi wa Kata ya Rau kuwa atasimama imara kuijenga Rau Mpya, sambamba na kurudisha imani ya wananchi kwa CCM na kumsaidia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025-2030.

