SHEKOLOA ASHINDA KURA ZA MAONI KATA YA KIUSA KWA KUPATA KURA 55.

Kauli Mbiu yake: "Kiusa Imara, Maendeleo Endelevu".


Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Kiusa, Manispaa ya Moshi, Khalid Shekoloa, ameibuka mshindi wa kura za maoni kwa kupata jumla ya kura 55.

Katika kinyang’anyiro hicho kilichoshirikisha wagombea watatu, Elizabeth Mushi alipata kura 24, huku Isack Munis (Gaga) akipata kura 13.

Ushindi wa Shekoloa unaashiria imani kubwa kutoka kwa wajumbe wa CCM Kata ya Kiusa, wakimtazama kama chaguo sahihi la kupeperusha bendera ya chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.