APAIKUNDA NABURI: ASHINDA KURA ZA MAONI KATA YA MAWENZI KWA KUPATA KURA 58


Kauli Mbiu: "Mawenzi ya Maendeleo, Kazi Iendelee"


Aliyekuwa diwani wa Kata ya Mawenzi, Apaikunda Naburi, ameongoza kwenye kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata jumla ya kura 58, akionesha kuungwa mkono kwa nguvu na wajumbe wa chama katika kata hiyo.

Katika kinyang'anyiro hicho cha kumpata mgombea wa udiwani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, wagombea wengine walikuwa Sulutani Mndema, aliyepata kura 26, na Mohammed, aliyepata kura 6.


Ushindi wa Naburi unatajwa kuwa ishara ya kutambua mchango wake wa awali kama diwani pamoja na imani ya wajumbe juu ya uwezo wake wa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Mawenzi kwa ufanisi na uadilifu.













Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.