APAIKUNDA NABURI AREJESHA FOMU YA UDIWANI KATA YA MAWENZI KUPITIA CCM

MOSHI-KILIMANJARO.

Mwanamama Apaikunda Naburi ameandika historia kwa kurejesha rasmi fomu ya kugombea nafasi ya Udiwani wa Kata ya Mawenzi, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Julai 2,2025 na Katibu wa CCM Kata hiyo, Joanitha John Byarushengo, amesema jumla ya watia nia wapatao 12 wakiwemo wanawake watatu na wanaume tisa waliojitokeza kuomba ridhaa ya chama hicho tawala ili kupeperusha bendera ya CCM kwenye nafasi ya udiwani, hatua inayodhihirisha kuimarika kwa ushiriki wa wanawake katika siasa za ngazi za msingi. 

Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Naburi amesema amechukua uamuzi huo kwa nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Kata ya Mawenzi kwa moyo wa kujituma, uwazi na kujali maslahi ya wengi.

“Nimeona ni wakati sahihi wa kuungana na wana CCM wenzangu katika kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi, niko tayari kushirikiana na kila mmoja kuhakikisha Kata ya Mawenzi inasonga mbele,” amesema kwa kujiamini.

Kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi ndani ya CCM, hatua inayofuata ni mchujo wa majina ya wagombea kabla ya kupitishwa kwa jina moja litakalowakilisha chama hicho katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.