AFRIKA-KUSINI
Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) kutoka Moshi, Tanzania, kimeshiriki kikamilifu katika maonesho ya kimataifa ya WoodEX for Africa 2025, yaliyofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 Juni 2025 katika ukumbi wa Gallagher Convention Centre, Johannesburg, Afrika Kusini.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Chuo cha FITI, Dkt. Lupala Zacharia, alisema kuwa maonesho hayo yalilenga kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya misitu, uchakataji wa mbao, fanicha na teknolojia za viwanda ili kubadilishana maarifa, kuonesha ubunifu wa kisasa, kuhamasisha ushirikiano wa kibiashara, na kukuza maendeleo endelevu katika mnyororo wa thamani wa misitu barani Afrika.
“Ushiriki huu ni sehemu ya mkakati wa FITI wa kuimarisha ubora wa mafunzo, kukuza teknolojia bunifu katika tasnia ya misitu, na kuweka Tanzania katika nafasi ya kimataifa inayotambulika kwa kuendeleza viwanda vya mazao ya misitu kwa njia endelevu,” aliosdema Dkt. Lupala.
Dkt. Lupala alisema katika maonesho hayo, FITI ilipata fursa ya kujifunza kuhusu teknolojia za kisasa za uchakataji wa mbao, matumizi ya mitambo mipya ya uvunaji na usindikaji, pamoja na mbinu bora za usimamizi wa misitu zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi na matumizi sahihi ya rasilimali.
Aidha, alisema ushiriki wa chuo hicho umetambua fursa mpya kwa vijana wanaosomea viwanda vya misitu, kwa kuwaonesha kwa karibu mahitaji ya soko la kimataifa na ujuzi unaotakiwa katika sekta hiyo, jambo linalosaidia kuwaandaa kushiriki ipasavyo kwenye mapinduzi ya viwanda vinavyotegemea misitu nchini Tanzania.
Kwa upande wake, Afisa Misitu kutoka FITI, Ignas Mambosasa, alisema kuwa ziara hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwa chuo hicho, hasa kwa wanafunzi wanaosomea teknolojia ya viwanda vya misitu.
“Vijana wetu watapata uelewa wa moja kwa moja kuhusu mahitaji ya soko la kimataifa na teknolojia zinazotumika leo hii kwenye uchakataji wa mazao ya misitu, hii itawasaidia kuwa na ushindani wa kweli katika soko la ajira na kuchangia kwa ufanisi katika maendeleo ya viwanda nchini,” alisema Mambosasa.
"Katika maonesho hayo, FITI ilipata fursa ya kujifunza kuhusu teknolojia za kisasa za uchakataji wa mbao, matumizi ya mitambo mipya ya uvunaji na usindikaji, pamoja na mbinu bora za usimamizi wa misitu zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi na matumizi sahihi ya rasilimali.
Aidha, ushiriki wa chuo hicho umetambua fursa mpya kwa vijana wanaosomea viwanda vya misitu, kwa kuwaonesha kwa karibu mahitaji ya soko la kimataifa na ujuzi unaotakiwa katika sekta hiyo, jambo linalosaidia kuwaandaa kushiriki ipasavyo kwenye mapinduzi ya viwanda vinavyotegemea misitu nchini Tanzania.
FITI pia ilishiriki katika mijadala ya kitaalamu kuhusu mustakabali wa sekta ya misitu Afrika, ikishirikiana na taasisi na wadau wakuu wa Afrika Kusini, wakiwemo:
Forestry South Africa (FSA), Sawmilling South Africa (SSA), Institute for Commercial Forestry Research (ICFR), South African Wood Preservers Association (SAWPA), South African Forestry Contractors Association (SAFCA), South Africa Forest Company Limited (SAFCOL), Council for Scientific and Industrial Research (CSIR) – Kitengo cha Misitu na Bidhaa za Mbao WoodBiz Africa
Pia aliyataja makampuni binafsi kama Mondi, Sappi, na York Timbers na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Afrika Kusini (FP&M SETA)
Dkt. Lupala aliongeza kuwa wadau hao walionesha nia ya dhati ya kushirikiana na FITI katika maeneo ya utafiti, ubadilishanaji wa maarifa, mafunzo ya kiufundi, na maendeleo ya teknolojia jumuishi katika tasnia ya misitu.
"Kupitia ushiriki huu, FITI imeweka msingi thabiti wa ushirikiano wa kikanda unaolenga kuinua ubora wa elimu ya kiufundi, kuongeza ujuzi wa kazi, na kupanua fursa za ajira kwa vijana wa Tanzania na Afrika kwa ujumla".














