WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA MKOA WA KILIMANJARO WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNUANI 'MEI MOSI'-2025



MOSHI-KILIMANJARO.

Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro, wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ ambayo Kimkoa yamefanyika katika Wilaya ya Moshi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).

Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, ambapo aliwasisitiza Wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu kwani serikali inawajali na kuwapenda.

Maadhimisho ya Mei Mosi 2025 yalikuwa na Kauli Mbiu isemayo ‘Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki’.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, akimkabidhi cheti  mfanyakazi bora kutoka Shirika la Posta Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro mwaka 2025 Afisa Daraja la Kwanza Charles Steven Lugendo.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.