WAFANYAKAZI WA MANISPAA YA MOSHI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI-2025

MOSHI-KILIMANJARO.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Bi. Mwajuma Nasombe, Mei 1, 2025 ameongoza wafanyakazi wa Manispaa hiyo kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kwa hamasa kubwa mjini Moshi.

Maelfu ya wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali ndani ya Manispaa hiyo waliungana katika maandamano yaliyotokea katika Ofisi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro (KNCU), na kuelekea Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), ambako shughuli zote za maadhimisho zilifanyika.

Katika hotuba yake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, aliwataka wafanyakazi kuendelea kushikamana na kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi ya wananchi na maendeleo ya taifa, huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha haki za wafanyakazi kazini.

“Siku hii ni ya kutafakari, kusherehekea, lakini pia kuhimiza uwajibikaji na uwazi mahali pa kazi,” alisema RC Babu.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu ya kitaifa isemayo: “Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki.”

Kitaifa, maadhimisho hayo yalifanyika mkoani Singida yakihusisha viongozi wa Kitaifa na wadau wa kazi kutoka sekta mbalimbali.

Siku ya Wafanyakazi Duniani huadhimishwa kila mwaka Mei 1, kama ishara ya kutambua mchango wa wafanyakazi katika kuendeleza uchumi na jamii.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.