Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro Jeremiah Mkomagi, akiwa katika maandamano ya amani na wanafunzi wa shule ya msingi Mwereni kuadhimisha siku ya Zimamamoto Duniani, kwa mkoa wa Kilimanjaro waliadhimisha siku hiyo kwa kufanya matembezi, kutoa elimu ya kinga dhidi ya majanga ya moto na mmatumizi ya namba ya dharura 114.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Mwereni wakiwa wamejumuika na askari wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro, kuadhimisha Siku ya zimamoto Duniani ambapo walifanya matembezi kutoka Makao makuu ya Jeshi hilo hadi Shule ya Msingi Mwereni.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji FC Albert Hamisho Mlugala, ambaye alikuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wa Manispaa ya Moshi wakati akiongoza maandamano hayo huku akitumia Pikipiki Maalumu.
Namna Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, walivyoadhimisho Siku ya Zimamoto Duniani, kwa kupita katikati ya mji wa Moshi wakitoa elimu ya kinga dhidi ya majanga ya moto na matumizi ya namba ya dharura ya 114 kwa wananchi wa Manispaa ya Moshi.












