MOSHI.
Thomas Lenana Marealle, alikuwa Mangi Mkuu Wa Wachagga Kuanzia Januari 1952 Baada Ya Kushinda Uchaguzi Uliohusisha Wagombea 4. Uongozi Wake Kama Mangi Mkuu Ulikuwa Wa Mafanikio Sana Kwani Uchaggani Kulikuwa Na Maboresho Mengi Katika Elimu, Afya, Miundombinu Ya Maji, Njia Za Mawasiliano, Katika Chama Cha Ushirika Na Ujenzi Wa Shule Na Vyuo.
Kabla ya kuwa Mangi Mkuu wa Wachagga Thomasi Lenana Marealle, alikuwa Meneja wa Programu wa Dar es Salaam Broadcasting Station (DBS) baada ya kutoka Masomoni Uingereza.
Lakini inasemekana alipuuza harakati za Chama Cha TANU na kusema bado hawajawa na uwezo wa kujiongoza na kwamba wanahitaji angalau miaka 25 mbele kuweza kujiongoza, inasemekana hakuwa na mahusiano mazuri na Nyerere na mwanzoni aliwapiga marufuku TANU kuingia Kilimanjaro.
Baada ya Uhuru wa Tanganyika hakujihusisha tena na Siasa za Nchi hii badala yake aliondoka na kwenda kufanya kazi Umoja wa Mataifa (UN) na kubakia huko mpaka kustaafu kwake.
Thomas Lenana Marealle, alizaliwa mwaka 1915 na kufariki 2007 akiwa na Umri wa Miaka 92, na kuzikwa huko Marangu, Lyamrakana.


