WAKRISTO WATAKIWA KUWEKA MSINGI WA KIIMANI KABLA YA KUHAMIA NYUMBA MPYA

MSAE-KINYAMVUO.

Wakristo amewakumbusha umuhimu wa kumshirikisha Mungu katika kila hatua ya maisha, hasa wanapopata mafanikio kama kujenga nyumba ya kuishi.

Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Mashariki la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Mchungaji Calvin Koola, aliyasema hayo Aprili 21,2025 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kuibariki nyumba mpya Chifu wa Marangu Frank Marealle, halfa iliyofanyika kijiji cha Msae Kinyamvuo kilichopo Kata ya Mwika Kaskazini Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mchg. Koola alisema kuwa ni vyema nyumba mpya ikakabidhiwa kwa Mungu kabla ya kuhamiwa, ili kuombewa baraka, amani na ulinzi wa Kiroho.

"Nyumba ni zawadi kutoka kwa Mungu, tunapojenga na kufanikisha ndoto hiyo, tusisahau kumshukuru na kumkabidhi yeye aliyeleta hayo mafanikio, kabla ya kuhamia, ni vyema kuiombea  nyumba hiyo kwa pamoja,"alisema Mchg. Koola.

Aliongeza kuwa msingi wa kiroho katika familia huanza nyumbani, hivyo kuifanya nyumba kuwa mahali pa baraka na si chanzo cha migogoro au changamoto za kiimani.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.