Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefanya
ukaguzi wa viwanja vitakavyotumiwa kufanyia mazoezi na timu zitakazoshiriki
michuano ya kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za ndani (CHAN) mwaka huu na
Kombe la mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027.
Majaliwa alifanya ukaguzi huo Machi
29,2025 Jijijini Dar es Salaamkatika viwanja vya Gymkhana. Meja Jenerali
Isamuhyo na kiwanja cha Chuo cha Sheria (Law School), vyote vilivyopo jijini
Dar es Salaam.
Michuano ya CHAN inayotarajiwa kuffanyika Agosti mwaka huu na AFCON mwaka 2027 , itapigwa katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.
Baada ya ukaguzi huo, Waziri Mkuu
Majaliwa aliwaagiza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Katibu Mkuu Wizara ya
Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na KAtibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu (TFF) kufanya tathmini ya kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja
vya mazoezi vitakavyotumika kwenye
michuano hiyo.
Alitoa maelekezo hayo baada ya
kupokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa SUMA JKT Brigedia Jenerali
Petro Ngata ambaye ndiyo Wakandarasi wa
mradi huo.
Majaliwa alisema ni vyema ufuatiliaji
wa karibu wa kila hatua za ujenzi na ukarabati ukafanyika ikiwa ni pamoja na
ukaguzi wa vifaa vyote ambavyo Mkurugenzi huyo amesema tayari vuimenunuliwa na
viko stoo.
Awali, Brigedia Jenerali Ngata ,
alimueleza Waziri Mkuu kuwa; kwa ujumla ujenzi na ukarabati umefikia asilimia
80 ya kazi kwa viwanja vyote ambavyo ni pamoja na ujenzi wa sehemu ya kuchezea
(pitch), vyumba vya wachezaji pamoja na
majukwaa.
Michuano ya Kombe la Afrika (CHAN)
inayoshirikisha Wachezaji wa ndani inatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 2 hadi
30 mwaka huu baada ya kuahirishwa mwaka
2024 huku michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) yanatarajiwa kufanyika
mwaka 2027.