Wafanyakazi NMB wafanikiwa kuifikisha Tuzo ya Mwajiri Kinara Mlima Kilimanjaro

MWEKA-KILIMANJARO.

Timu ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB wamefanikiwa Kuifikisha Tuzo ya Mwajiri Kinara, katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Akizungumza katika hafla ya mapokezi iliyofanyika katika lango la Mweka, Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu NMB Jeseph Ngalawa, aliishukuru timu hiyo kuwa kuweza kuifikisha bendera na Tuzo hiyo, ambayo walikabidhiwa kama Mwajiri Kinara Tanzania.

Alisema ili uweze kupanda mlima Kilimanjaro inahitaji ustahimilivu wa hali ya juu, ushirikiano wa dhati na dhamira thabiti hivi ndio vitu ambavyo vinahitajika pia hata katika utekelezaji wa majakumu  kama Benki ya NBM na ndio vitu ambavyo vimepelekea Benki ya NBM kutambukila kama Mwajiri bora hapa nchini.

Alisema Benki ya NMB  waliona ni jambo zuri kuipeleka Tuzo hiyo Mlima Kilimanjaro, kwa sababu ni Mlima unaotambuliwa Kimataifa.

Akizungumza kiongozi wa waliopandisha bendera na Tuzo ya Mwajiri Kinara Meneja wa NMB Ngalenaro Limbris Israel, alisema jumla ya watu wanne waliopanda mlima huo wote wamefanikiwa kufika katika kilele cha mlima Kiliamnajro.

Akizungumzia changamoto ya kuupanda mlima huo Israel alisema; baadhi ya watu wengi wanahofu kubwa ya kuupanda mlima huo mrefu barani afrika kutoka na kupewa historia za mlima wenyewe kwa jinsi ulivyo.

Naye Afisa Masoko kutoka Kampuni ya utalii “Zara tours Adventure” Nance Ngotea; aliishukuru Benki ya NMB kwa kuichagua kampuni hiyo kuweza kuwapandisha wafanyakazi hao.

















Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.