MOSHI.
Mkoa wa Kilimanjaro umepokea dozi milioni 3.4 dhidi ya magonjwa ya mapafu ya Ng’ombe, mdomo wa kuku na sotoka ya mbuzi na kondoo.
Katibu Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Kilimanjaro Dk. Emmanuel Lema, aliyasema hayo wakati akitoa taarifa ya Mifugo na Uvuvi kwa Wajumbe kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mkoani hapa.
Dk. Lema alisema Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilinunua chanjo hizo pamoja na vifaa vya kuchanjia mifugo dhidi ya magonjwa ya mapafu ya ng’ombe (CBPP) na kideri, mdomo wa kuku na Sotoka ya Mbuzi na Kondoo.
“Mkoa wetu umepokea Jumla ya Dozoi milioni 3.4 kati ya hizo dozi za kuku ni milioni 1, 700,000 , dozi za mapafu ya ng’ombe 492,700 dozi za Sotoka ya mbuzi na kondoo milioni 1,212,800,”alisema Dk. Lema,”alisema.
Dk. Lema aliwaomba Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wasaidie kuhamasisha wafugaji kupeleka mifugo yao kwa ajili ya kupata chanjo ili zoezi hilo liweze kufanyika kwa mafanikio makubwa.
Aidha alisema Serikali kupitia Wizara ya Kilimo katika msimu wa mwaka 2024-2025 imeendelea kutoa ruzuku za mbolea kwa Wakulima kote nchini, ambapo imeongeza ruzuku kwenye mbegu za mahindi.
“Ili mkulima anufaike na mbegu hizi anatakiwa kujisajili kwenye mfumo wa mbolea za ruzuku zoezi la usajili kwa Wakulima ambao hawajajisajili linafanywa na maafisa ugani wetu wa kilimo kuanzia ofisi za kijiji, kata, halmashauri na hata shambani kwa kutumia vishikwambi walivyopatiwa na serikali”alisema Dk. Lema.
Alisema vitu muhimu ambavyo mkulima anatakiwa kuwa navyo ni pamoja na kitambulisho cha NIDA au cha mpiga kura, awe na shamba analolimiliki yeye mwenyewe au la kukodi.
“Tunawaomba Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi mtusaidie kuwahamasisha wananchi kupitia vikao na mikutano yenu mbalimbali, ili wananchi na Wakulima kijisajili kwenye mfumo wa ruzuku za mbolea maana mfumo huo ndio utakaomwezesha mkulima kuweza kununua mbegu za mahindi zenye ruzuku na hakutakuwa na dula la pembejeo litakalouza mbegu hizo nje ya mfumo.”alifafanua.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu mkoani humo Stephen Kivulenga, akatoa tahadhari kwa wakazi mkoani hapa kuhusu mwelekeo wa mvua za msimu wa masika kuanzia zinazotarajiwa kuanza kunyesjha mwezi Machi hadi Mei mwaka huu.
“Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, imetoa mwelekeo wa mvua za msimu wa masika kwa kipindi cha Machi hadi Mei, ambapo ni mahususi kwa mikoa ambayo inapata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.”alisema.
Alisema mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu hadi mwezi Mei, ambapo ongezeko la mvua hizo zinatarajia kuwa mwezi wa Aprili mwaka huu.
“Kutokana na mwelekeo wa mvua hizo kuna uwezekano wa kutokea kwa mafuriko na vipindi vya unyevu wa udongo kuzidi na hivyo kusababisha kuwepo kwa maporomoko ya ardhi na kuzomba Kamati za Maafa za Wilaya kuhakikisha wananchi wote waishgia maeneo ya milimani na kwenye mabonde kuanza kuhama.”alisema.
.jpg)







.jpg)
.jpg)