Kampeni ya Samia yatatua migogoro 94 Kilimanjaro

MOSHI.

Jumla ya migogoro 740 imewasilishwa  wakati wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) mkoani Kilimanjaro, ambapo kati yake 94 imetatuliwa papo hapo wakati 646 ikiendelea kushughulikiwa.

Mratibu wa Kampeni hiyo kwa mkoa wa Kilimanjaro Wakili wa serikali kutoka Wizara ya katiba na Sheria Murumbe James Daudi, alibainisha hayo jana wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kampeni hiyo kwa  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu.

Alisema migogoro hiyo iliwasilishwa na wananchi kwenye maeneo yaliyofikiwa na kampeni hiyo na takribani wananchi 121,349 walifikiwa.

“Kati ya migogoro 740 iliyowasilishwa wakati wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) mkoani Kilimanjaro, kati yake migogoro 94 ilitatuliwa papo hapo huku migogoro ya ardhi kati ya 6 hadi 15 tuliweza kuitatuamoja kwa moja,”alisema.

Alisema mwananchi alipokuwa akifika ttulikuwa tunampa ushauri , utaratibu afanyeje kama jambo lake lilishahitimishwa mahakamani na wengi walituelewa.

Alisema kampeni hiyo pia iliambatana na huduma ya usajili chini ya Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na wananchi zaidi ya 500 walifikiwa na huduma hiyo.

“Tunashukuru sana Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano tuliopewa kufanikisha kampeni hii,kwani malengo ya Wizara yametimia katika ka, vijiji na mitaa iliyokuwa imepangwa kufikiwa wakati wa kampeni hii yote imefikiwa,”alisema wakili Daudi.

Aidha Mratibu huyo alitumia fursa hiyo pia kuwataka wannanchi mkoani humo kuendelea kuwatumia viongozi wa Serikali kupitia ofiosi za serikali zilizopo kwenye maeneo yao kwa klufika katika ofisi hiyo ili kuweza kuwasilisha changamoto zao.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la wlimu Wazalendo Manispaa ya Moshi Rashidi A. Rashidi, alimshukuru Rais Sami kwa kuwaleta wasaidizi wa Kisheria mkoani hapa, kwani wananchi wengi hasa wenye kipato cha chini walikuwa wakishindwa kuweka mawakili kusimamia kesi zao.

“Kesi nyingi zilikuwa zikichukua muda mrefu kwa kukosa fedha za kuwalipa mawakili, lakini Rais Samia kwa kuleta wasaidizi wa kisheria wameweza kuwatatulia kezi zao,”alisema Rashidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha kampeni hiyo kwani imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.