Wakili wa Serikali Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Kilimanjaro Tamari Mndeme, akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake kuelekea uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Kisheria, hafla itakayofanyika Januaria 21, 2025.
MOSHI-KILIMANJARO
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, anatarajiwa kuzindua Kamati ya Ushauri wa Kisheria, huku wananchi
wakitakiwa kuhakikisha wanafika katika kliniki hiyo na kupata elimu ya sheria
ili itakayotolewa bure kwa kipindi cha wiki moja kuanzia Januari 21hadi januari 27 mwaka huu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ushauri wa Kisheria mkoa wa
Kilimanjaro Tamari Mndeme, aliyasema hayo Januari 19, 2025 wakati akizungumza
na waandishi wa habari ofisni kwake.
Alisema
baada ya kuzinduliwa kwa Kamati hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Kamati hiyo itaanza
rasmi kazi ya kuendesha kliniki hiyo, ambayo itakuwa imesheheni maofisa kutoka
taasisi mbalimbali za serikali.
“Kliniki
hii itafanyika kuanzia Januari 21, mwaka huu katika viwanja vya stendi kuu ya
mabasi Moshi, nawashauri wananchi kuitumia
fursa hii adhimu ili waweze kuja kupata ushauri wa kisheria ambao utawasaidia
kutatuliwa kwa changamoto zao,”alisema.
Mndeme
ambaye pia ni Wakili wa Serikali Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoani humo, alisema wananchi wamekuwa na
malalamiko na migogoro mingi inayohusu mambo ya kisheria na hawajui sheria na kuwataka
kuitumia wiki hiyo ya sheria.
“Kesi
nyingi zinazowasilishwa na wananchiwa mkoani humo, zinahusiana na masuala ya
ardhi, mirathi, ukatili, ndoa na masuala mengine ya kijamii.”alisema.
Katibu
wa Kamati ya Ushauri wa Kisheria mkoa wa Kilimanjaro, Kisa Lyimo, alisema
programu ya msaada wa kisheria, imeanzishwa kwa madhumuni ya kuwasaidia
wananchi kupunguza migogoro na malalamiko ya kisheria yanayowakabili.
Nao
baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Moshi Msumari Simoni, Adam Seif na Mwl Japhet
Mpande, walisema ujio wa kliniki hiyo utawasaidia kuwatatulia changamoto
zinazowakabili ikiwemo migogoro ya ardhi.
Timu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika mkutano na Wakili wa Serikali Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Kilimanjaro Tamari Mndeme hayupo katika picha, kuzungumzia uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Kisheria, inayotarajiwa kufanyika Januaria 21, 2025.

