MOSHI-KILIMANJARO.
Uongozi wa serikali ya mkoa wa Kilimanjaro umeahidi kuhakikisha uanimarisha usalama wa mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2025, zinazotarajiwa kufanyika Februari 23, mwaka huu.
Mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon zijulikanazo kama Kili Marathon hufanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi Februari mjini Moshi katika mkoa wa Kilimanjaro ambapo kwa mwaka huu zinatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 12,000 kutoka nchi takribani 56.
Akizungumza Katibu Tawala wa mkoa huo Kiseo Yusuf Nzowa, kwenye uzinduzi wa msimu wa 23 wa mbio hizo, lisisitiza kuwa serikali imejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama kwa washiriki, wadhamini na wadau wote watakao shiriki katika tukio hilo kubwa.
Aidha Katibu Tawala huyo ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Manispaa na Moshi vijijini, kuhakikisha mji wa Moshi unakuwa msafi wakati wote wa mbio hizo ili kuepuka hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Tanzania mkoa wa Kilimanjaro Nelson Mrashan, amewashukuru wadhamini wote ambao wameendelea kudhamini mbio hizi, huku akiahidi kuendelea kuwaunga mkono.
Mrashan; amesema kwa mwaka huu chama hicho kimeandaa Kalenda ya kila wilaya ya mashindano ya mbio za marathon lengo likiwa ni kuwaandaa vijana watakaokuwa wakishiriki mbio hizo.
Aidha mwenyekiti huo ametoa ombi kwa Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro, kwapatia eneo ambalo watajenga kituo michezo, kwani wako wadau wengi ambao wamekuwa wakishiriki mbio hizo za Kilimanjaro Marathon kutoka mataifa mbalimbali, kusaidia ujenzi wa kituo hicho.
Zaidi ya watu 12,000 kutoka mataifa 56 mbalimbali wanatarajiwa kushiriki mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon zitakazofanyika Februari 23 mwaka huu.








