MOSHI-KILIMANJARO.
Chama cha Mafundi Rangi na Ujenzi Mkoa wa Kilimanjaro (CHAMARUKI), kimewashukuru wadau wa elimu Magic Builder's International Ltd, inayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa za ujenzi kama vile white skim wall putty, kwa kusaidia kuwalipia ada watoto 150 wa mafundi rangi na ujenzi wanaosoma shule za msingi za serikali mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Katibu wa CHAMARUKI Casmiry John Toto, wakati akizungumza na Kisenaupdateblogger katika mahojiano maalumu, alisema wadau hao wa elimu, wamekuwa wakishirikiana na serikali kwa lengo la kusaidia wanafunzi hasa watoto wa kike kwenye suala la elimu.
Katibu huyo alifafanua kuwa, CHAMARUKI mbali na kulenga kuwaunganisha mafundi hao ili waweze kupaza sauti kwa pamoja, sambamba na kuunda mfumo utakaowezesha usimamizi bora wa kazi na kutoa fursa za kibiashara kwa mafundi hao kupitia ushirikiano na serikali, pia kinalenga kuwakutanisha na wadau mbalimbali kutatua changamoto mbalimbali wanazokukumbana nazo.
“Katika mkutano mkuu wetu wa kwanza wakjo wadau wa elimu walijitokeza kuwasaidia kuwalipia ada za shule watoto wao wanaosoma shule za msingi za serikali, napenda kukuambia kuwa zaidi ya wanafunzi 100 kutoka wilya ya Siha, Moshi vijijini, Hai Same na Manispaa ya Moshi wanakwenda kunufaika na fursa hiyo kwa kulipiwa ada kwa mwaka mzima,”alisema Toto.
Akifungua Mkutano wa chama hicho hivi karibuni, Katibu Tawala Wilaya ya Moshi Shaban Mchomvu, aliwashukuru wadau hao Magic Builder's International Ltd, kwa kuwasaidia wanafunzi kulipia ada ili waaweze kusoma.
“Niwashukuru sana Magic Builder's International Ltd, kwa kuiunga mkono serikali katika suala la elimu kwa kuwasaidia wawazi wa watoto hawa kuwalipia karo ya shule,”alisema Mchomvu.
Katika Mkutano huo, Kampuni ya Magic Builder's International Ltd, inayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa za ujenzi kama vile white skim wall putty,iliahidi kuwalipia ada watoto wa mafundi rangi na ujenzi wanaosoma shule za msingi za serikali.
Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Kaskazini, Brighton Geofrey, alisema hatua hiyo ni sehemu ya kutambua mchango wa mafundi hao katika kufanikisha malengo ya kampuni hiyo.
Kwa upande mwingine, alielezea kuwa kampuni hiyo ina mipango ya kuendelea kusaidia mafundi rangi na ujenzi, na kwamba wameanzisha mpango huu katika mkoa wa Kilimanjaro kama sehemu ya michango yao kwa jamii.


,%20wakiwa%20katika%20Mkutano%20Mkuu%20wa%20Kwanza%20wa%20chama%20hicho..jpg)
%20Brighton%20Geofrey,%20akiwa%20katika%20mkutano%20wa%20CHAMARUKI..jpg)
