Serikali yawaonya madereva wanaolaza magari ya serikali kwa magirlfriend, baba wakwe

MOSHI-KILIMANJARO

Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Kiseo Nzowa, amewaonya madereva wanaoendesha magari ya serikali muda wa saa za kazi unapomalizika kuchukua magari hayo na kwenda kuyalaza kwa wapenzi wao (Girlfriend) au kwa Baba wakwe jambo ambalo ni kinyume na utaratibu cha maadili ya sheria za Utumishi wa umma

Nzowa aliyasema hayo 26,2025 kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST) Mkoa wa Kilimanjaro,uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uhamiaji Kikanda  (TRITA) mjini Moshi mkoani humo.

Amesema kuwa wako baadhi ya madereva wa serikali pale muda wa saa za kazi unapomalizika huchukua magari hayo na kwenda kuyalaza kwa wapenzi wao (Girlfriend) au kwa Baba wakwe kinyume na utaratibu.

Alisema utaratibu wa kulaza magari ya serikali baada ya saa za kazi unafahamika,lakini wako baadhi ya madereva hawazifuati taratibu hizo na kwenda kuyalaza kwa wapenzi wao.

Aidha alisema wako baadhi ya madereva muda wa kazi unapokwisha, huchukua magari ya serikali na kwenda kubebea majani ya mifugo, huku wengine wakienda kubeba magunia ya mkaa na mchanga jambo ni kimyumbe na maadili ya utumishi wa umma.

Aidha Nzowa alitoa maelekezo kwa madereva hao wanapokuwa na viongozi wao katika magari, wajitahidi sana kutunza siri kwa kuwa wanabeba  dhamana ya nyaraka za serikali.

Pia Katibu Tawala huyo, aliwataka madereva hao kujiepusha na ulevi, huku pia akiwataka kuwa nadhifu wanapokuwa kwenye eneo lao la kazi.

Akifungua Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, alitoa maelekezo kwa Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna msaidizi wa Polisi  ACP Nassoro Sisiwaya, kuhakikisha kwamba dereva yeyote wa serikali atakayebainika amevunja sheria za usalama barabarani achukuliwe hatua.










Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.