Waziri Pindi Chana mgeni rasmi ufunguzi Tamasha la “Same Utalii Festival Season-Two”


MOSHI-KILIMANJARO

Waziri wa Maliasili ya Utalii Balozi, Dk. Pindi Chana, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Tamasha la “Same Utalii Festival Season-Two, litakalofanyika Desemba 21 mwaka huu katika viwanja vya Standi Kuu ya Same Wilayani humo.

Taarifa hiyo imetolewa Desemba 18,2024 na Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Jeremiah Mgeni, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi mkoani humo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema, baada ya Waziri Chana kuwahutubia wananchi watalii, ataelekea hifadhi ya Mkomazi, kutembelea vivutio vya utalii, ikiwemo mlima  kidenge, lengo likiwa ni kuibua vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya  Wilaya hiyo.

DC Mgeni, amesema mtalii anapo ukwea mliama Kidenge, anaweza kuona mawio na machweo ya jua vizuri anapokuwa juu ya kilele hicho, hayo, chura ambaye hapatikana sehemu yoyote duniani, punda, wataona mapango, rupia, pia watalii wataweza kuwaona ng’ombe ambao wanaishi kwenye mapango, lakini pia mlima huo ni mzuri na una kona nzuri.

Aidha amesema Desemba 22, mwaka huu watalii watatembelea hifadhi ya Msitu wa Shengena, ambapo wataweza kumuona ndege aliyechorwa uwanja mweupe, pamoja na  miti ambayo haipatikani maeneo mengine yoyote, huku akitaja kivutio kingine kuwa ni upepo mkali unapokuwa katika msitu huo.

Vile vile amesema Usiku wa desemba 22, kutakuwa na tamasha la wanamziki mbalimbali akiwemo mwanamuziki wa Singeli Jay Combat, Msanii wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan maarufu (Tunda Man) pamoja na wasanii wengine wa ndani kutoka wilaya ya Same, ambapo pia kutakuwa na nyama choma Festival kutoka Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa tamasha hilo litazinduliwa rasmi na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdi Babu, Desemba 20 mwaka huu na kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho yatakayokuwa katika viwanja vya Standi kuu ya mabasi Same.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.