MOSHI-KILIMANJARO.
Mkuu wa Wilaya ya Same
Kaslida Jeremiah Mgeni, amewaalika wawekezaji kuja kuwekeza kwenye Sekta ya
Utalii kwa kujenga hoteli zenye hadhi.
Hatua hiyo inakuja kutokana
na Wilaya hiyo kuwa na wageni wengi wanaokuja kutembelea, Hifadhi ya Taifa ya
Mkomazi, kupitia mradi wa Mbwa mwitu na
Faru ndani ya hifadhi hiyo ambao umefanya idadi ya wageni kuongezeka kwa
asilimia 100 kwa mwaka.
Akizungumza na waandishi wa
habari mjini Moshi, kuhusiana na Tamasha kubwa linalojulikana kama “Same Utalii
Festival” ambapo tamasha hilo litafanyika Disemba 20 hadi 22 mwaka huu.
Kasilda amesema kukosekana kwa
hoteli zenye hadhi, baadhi ya watalii wanalazimika kwenda kulala Moshi,
kutokana na ukosefu wa hoteli zenye viwango na kutoa rai kwa wafanyabiashara
kuja kuwekeza kwa kujenga hoteli zenye hadhi ili watalii wanapokuja kutembelea
hifadhi hiyo wasipate adha ya kupata mahali pa kulala.
Amesema tangu kuanzishwa
kwa Tamasha la Same Utalii Festival, wawekezaji wamehamasika kuja kuwekeza kwa
kujenga hoteli zenye hadhi, ambapo mwekezaji mmoja amejenga hoteli kwenye lango
la kuelekea Mkomazai huku hoteli mbli zikijengwa kwenye mlima wa hifadhi ya
Shengena moja wapo ikiwa ya nyota tano.
“Tamasha la Utalii Festival, imekuwa na tija
kubwa, limeongeza ajira kwa vijana, hoteli zinazojengwa ajira zitaongezeka,
waongoza watalii wengi wataongezeka, kupitia vivutio vya utalii ulivyoko wilaya
kwetu.”amesema.
Aidha amesema idadi ya
watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi imeongezeka ambapo kwa mwaka
2023 takribani watalii 7,000 walitembele hifadhi hiyo na kwamba baada ya
tamasha hili kufanyika idadi imeongezeka na kufikia watalii 10,000.
“Baada Tamasha la Utalii Festival-one, hadi sasa
idadi ya watalii imeongezeka
kutoka watalii 7000 hadi kufikia watalii 10,000 jambo ambalo limeleta
matumaini makubwa sana kwa wananchi wa Same,
Ameongeza ”Kuwepo kwa mradi
wa Mbwa mwitu na Faru, imekuwa ni
kivutio kikubwa cha utalii, hususan watalii kutoka nje ya nchini, ambao
wamekuwa wakitembelea hifadhi hiyo kutokana na
uwepo wa vivutio hivyo.”amesema.







