SIHA-KILIMANJARO.
Mkurugenzi wa Hospitali Maalum ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto (KIDH) Dk. Leonard Subi, amekutana na watumishi wa sekta ya afya, pamoja wafanyakazi wa kada mbalimbali wakiwemo walinzi na kuwazawadia kilo 10 za mchele kila mmoja, ili kila mfanyakazi awe na wakati mzuri wa kukaa na familia yake kipindi chote cha Sikukuu ya Krimas.
Dk. Subi, amesema zawadi hiyo ameitolewa kwa wafanyakazi hao, ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza kutokana na huduma bora wanazozitoa kwa wagonjwa wanaofika kutibiwa hospitalini hapo.
“Huu ni utaratibu wetu wa kila mwaka wa kukutana na wafanyakazi wa taasisi, pamoja na uongozi wa juu wa taasisi yetu, ili kukumbushana yale yote waliyoyafanya kwa mwaka mzima.”amesema Dk. Subi.
Amesema wamekuwa na utaratibu huo wa kila mwaka wa kukutana na wafanyakazi wote, ili kutafakari kazi walizozifanya kwa mwaka mzima pia kuzawadiana ikiwemo vyakula ili kila mfanyakazi awe na wakati mzuri na familia yake katika kipindi chote cha Sikukuu na leo nimewapatia kila mtumishi kilo 10 za mchele huku akiwatakia Heri ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya 2025 wenye mafanikio mema.”amesema.
Aidha Dk. Subi, amewataka watumishi wa hospitali hiyo, kuongeza juhudi katika sehemu zao za kazi, ili hoospitali ya Kibong’oto, iendelee kuwa namba moja katika kutoa huduma mbalimbali za afya.
Akiongea kwa niaba ya wafanyakazi wenzake kwenye hafla hiyo, mmoja wa wafanyakazi hao Saidi Omari, ameushukuru uongozi wa hospitali hiyo kwa zawadi hizo ambapo amesema uamuzi wa uongozi wa hospitali hiyo kuwazawdia kipindi hiki cha Sikukuu utawapa ari ya kuendelea kuwahudumia watu wanaokwenda hospitalini hapo kupata huduma mbalimbali.