Watu wenye ulemavu Wapanda Mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru kuonyesha uwezo wao


MOSHI-KILIMANJARO

Watu wenye ulemavu  wa aina mbalimbali wakiwemo wenye ulemavu wa ngozi (Albino), viziwi na wenye uoni uoni hafifu, wameamua kupanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika.

Safari yao ya kukwea mlima huo Mrefu Barani Afrika ilianza Desemba 5, mwaka huu, kupitia njia ya Marangu, ambapo watu hao wanatarajiwa kufika kilele cha Mlima huo maarufu Uhuru Park Desema 9, 2024. kushuka desemba 10, 2024.

Akizungumza  na Waandishi wa habari kabla ya kuanza safari yake ya siku tano, mmoja wa watu wenye ulemavu wa macho Siwema Hamisi, amesema  wamepata fursa ya kukwea  wamlima huo ili kutoa ujumbe kwa dunia kwamba licha ya ulemavu walionao, wana uwezo wa kufanya jambo lolote.

“Tangu akiwa mtoto mdogo, nilitamani sana siku moja na mimi niweze kupanda mlima Kilimanjaro, nashukuru kwa  kupata fursa hii ya kuwa miongoni mwa watu ambao nipanda mlima Kilimanjaro....nipende kuwahakikishia Watanzania wenzangu kwamba nitaukwea mlima huu hadi kilele na kuisimika Bendera ya Taifa.

Siwema, amesema licha ya ulemavu alionao, atakwenda kuwashangaza Watanzania ambao hawana ulemavu kuwa, ulemavu sio mwisho wa maisha lakini pia kupanda mlima ni njia nzuri ya kuwaonyesha watu wsio na ulemavu kwamba tunajitegemea na tunaweza.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la (Action For Persons With Disability), linalohudumia watu wenye ulemavu Tanzania, Mjumbe wa Bodi hiyo Stephen William, amesema kuwa kupanda mlima ni njia ya kuhamasisha utalii wa ndani na pia kipimo cha afya, huku akisistiza kwamba lengo la safari hiyo ni kuonyesha kuwa ulemavu hauwezi kuwa kizuizi kwa mtu kufikia malengo yake.

“Hatua hii pia inaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akihamasisha Watanzania kupitia filamu yake The Royal Tour ili wajiunge na harakati za kupanda Mlima Kilimanjaro na kuhamasisha utalii wa ndani.” Amesema William.

Ameongeza kuwa Kwa ujumla, ni safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwao ina maana kubwa sana, kwani inathibitisha uwezo wa watu wenye ulemavu na inaongeza umuhimu wa kujivunia taifa letu na utalii wake.

“Hakuna kizuizi kinachoweza kuzuia mtu kufikia malengo yake, hata kama ana changamoto za kimwili. Watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali, wakiwemo viziwi, albino, na wenye uoni hafifu, tunapanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika na kutoa ujumbe kwa dunia kwamba tunao uwezo wa kufanya mambo makubwa.”amesema.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.