Wanafunzi kidato cha tatu shule ya sekondari New Dawn, wamwaga machozi wakiimba shairi la kuwaaga kidato cha nne

Wanafunzi wa Kidato cha Tatu, Shule ya Sekondari New Dawn iliyopo Kata ya Njoro, Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, wakiimba Shairi la kuwaa Wanafunzi wa kidato cha Nne kwenye Mahafali ya Tatu toka kuanzishwa kwa shule hiyo Mwaka 2019

1. Hodi hodi twaingia, ingawa twahuzunika,

Wakati umewadia, hatuwezi zuilika

Tamati imefikia, mwarudi mlikotoka

Kwaherini, Twaaga, New Dawn mwakaribishwa.

2. Sisi tunawaageni, mikono twawapungia,

Ila twatoa maoni, usia wetu sikia, na mkiufuateni, faida tajipatia

Kwaherini twaaga New Dawn Mwakaribishwa.

3. Mkatulie nyumbani kasi epuka safari,

Kila siku munjani, mkidandia magari,

Watakuita muhuni, jina hili ni hatari

Kwa herini twaaga, New Dawn mwakaribishwa.

4. Nawe Seba kaka yetu, mkuu wa msafara

Leo hii pigo kwetu, kutuacha ni hasara

Lini utakuja kwetu, utulishe ya busara

Kwa herini twaaga, New Dawn mwakaribishwa

5. Usafiri kwa salama, ewe Kaka yetu Mosha,

Njiani usijekwama, ukalisukuma gari

Nyumbani fika salama, mkapashane habari,

Kwa herini twawaaga, New Dawn mwakaribishwa

6. Wewe Queen tunakuaga, kwa heri ya kuonana,

Tutakuja kukutana, akipenda maulana,

Na tumefahamiana, popote tutakutana

Kwa herini twaaga, New Dawn mwakaribishwa

7. Jack kutuhamasisha, sheria kutuongoza,

Juhudi ulituonyesha heshima kutuongoza;

Amani kuhamasisha, kwa pamoja tuliweza;

Kwa herini twaaga , New Dawn mwakalibishwa

8. Kaka zetu twaombeni, mkazidishe nidhamu,

Wakubwa kaheshimuni, pia mkwasalimu

Usijeenda ukweni, mkaiacha elimu,

Kwa herini twaaga, Ne Dawn mwakaribishwa

9. Enyi dada zetu pia, muende mjiheshimu,

Wazazi kusaidia na ndugu kuwaheshimu;

Manani kuyatilia, mlopewa na walimu

Kwa herini twaaga , New Dawn mwakaribishwa

10. Mwisho twasema poleni; kama tuliwakosea,

Usia ukumbukeni, msije kupuuzia,

Mtakumbuka mbeleni, yatakapowatokea

Kwa herini twaaga New Dawn mwakaribishwa.














Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.