MANISPAA-MOSHI
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, mkoa wa Kilimanjaro,
imemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapandisha madaraja Watumisi zaidi
ya 1000 na kuwalipa malimbikizo yao ya mishahara.
Taarifa ya Serikali kuhusu kupandishwa madaraja watumishi na
kuwalipa malimbikizo ya mishahara, imetolewa jana na Mkurugenzi mtendahi wa
Manispaa hiyo Mwl. Mwajuma Nasombe, wakati akizungumza na Watumishi wa Manispaa
hiyo.
Amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 Rais
Samia ameruhusu, upandishwaji wa vyeo
kwa watumishi 1,071, ajira mpya 54 na kubadilishwa vyeo watumishi 61.
“Sisi watumishi wa Manispaa ya Moshi, tunamshukuru sana Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapatandisha
madaraja watumishi zaidi ya 1, 000 kwa
kipindi akiwa madarakani, pia tunamshukuru kwa kuleta ajira mpya 54 ndani ya Manispaa
yetu ya Moshi , kubadilisha vyeo
watumishi 61 ambapo huko nyuma ilikuwa njozi na sasa chini ya Rais Dk. Samia imewezekana.”amesema Mwl. Nsombe.
Mwl. Nasombe amesema Serikali kuwapatia stahiki zao, inataongezea watumishi morali ya kufanya kazi na kuondoa manung’uniko
na visingizio vya viporo kazini, huku akiwataka watumishi hao kufanya kazi kwa
ari zaidi ili kuifanya Manispaa iendelee kupiga hatua zaidi.
Aidha Mkurugenzi huyo, amepiga marufuku kwa mtumishi yeyote wa umma, kufika
kazini akiwa amelewa au kutumia vilevi
wakati wa kazi, na kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika, ikiwa ni
pamoja na kuondolewa kazini.
Mwl. Nasombe,
ameyataja matumizi ya vilevi kazini ni mojawapo
ya mifano ya utovu wa nidhamu, huku akisema kuwa ni aibu kwa mtumishi wa umma
ambaye anadhihirisha tabia za kulewa, huku akieleza kuwa nidhamu ni nguzo
muhimu ya mafanikio katika utendaji kazi.
“Nidhamu, inahusisha pia kuheshimu taratibu, viongozi, na
wenzao kazini, uzembe, tabia mbaya, na uvunjifu wa maadili ni baadhi ya mifano
ya utovu wa nidhamu, ambayo inaweza kusababisha kuvunjwa kwa kanuni za kudumu
za utumishi wa umma za mwaka 2009.”amesema.
Mkurugenzi huyo, pia aliwataka watumishi wa halmashauri ya
Manispaa hiyo, kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana ili kazi katika
idara ziweze kufanyika kwa ufanisi.
Akizungumzia suala la uwajibikaji Mwl. Nasombe, amesema ni
moyo wa utendaji bora, ambapo kila kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha
anatimiza majukumu yake kwa uaminifu na weledi.
“Serikali ilianzisha mfumo wa upimaji, utendaji kazi kwa
watumishi na upimaji wa taasisi (PEPMIS) ambayo sasa inajulikana kama mfumo wa
e-Utendaji, ili kila mtumishi aweze kuingiza mipango yake ya kazi na kisha
kutoa taarifa za utendaji wa kazi hizo kwenye mfumo, kulingana na mpango ambao
kila mtumishi ameingia.
Ameongeza kuwa “Jambo la kusikitisha ni kwamba amepokea
orodha ya watumishi ishirini na nane (28) ambao hadi sasa hawajaingiza mpango
wao wa kazi katika mfumo huo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, watumishi hao
wameshindwa kuwajibika kwa kutotii maelekezo ya serikali na wanastahili
kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuvunja kanuni za utumishi wa umma za mwaka
2022 kanuni 42 (8) ikisomwa pamoja na kanuni za kudumu za utumishi wa umma za
mwaka 2009.
Nao baadhi ya
watumishi wa halmashauri hiyo, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa
kuwapandisha madaraja watumishi na kuwalipa mishahara yao, huku wakimuomba
kuendelea kuwaona zaidi.





