FUKA-SIHA
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania
Mentors Action Dk. Paul Nandrie, ameongoza maelfu ya wananchi katika mashindano
ya riadha yajulikanayo kama Siha Marathon 2024, yaliyofanyika katika Viwanja
vya Fuka Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza mara baada ya
kumaliza mbio za hizo Dk. Nandrie, ameisisitiza jamii umuhimu wa kufanya
mazoezi mara kwa mara, kama njia bora ya kuepuka magonjwa yasiyo ya
kuambukizakama vile shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo, kisukari,
magonjwa ya figo na kifua kikuu TB.
Amesema kuwa jamii inapaswa
kujiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi ikiwa ni pamoja na kushiriki katika mbio
kama hizo ili kupunguza hatari ya kupata magonjwa hayo.
“Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa
ni mengi sana, ili kuyatokomeza magonjwa kama haya yataondolewa kwa kufanya
mazoezi ya mara kwa mara,”amesema Dk. Nandrie.
Kwa upande wake Mkurugenzi
mtendaji wa halmashuri ya Siha Dk. Haji Mnasi, amesema mbio za Siha Matrathon, zimekuwa
na manufaa makubwa ambapo zimekuwa zikiwa kutanisha wadau kutoka maeneo
mbalimbali kuja kushiriki mbio hizo.
Aidha Dk. Mnasi, amewataka waandaaji
wa mbio hizo, kujipanga zaidi kwa msimu ujao, ili wananchi na wadau mbalimbali
waweze kushiriki kwa wingi katika msimu ujao.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Duncan
Urassa, amesema mbio hizo, zimekuwa zikisaidia kujenga afya na kuvitangaza
vivutio vya utalii Wilayani humo.
“Ukosefu wa mazoezi ya mara kwa mara, huchochea magonjwa yasiyo ya kuambukiza, hivyo mbio hizi zimetusaidia sana kujenga afya zetu,”amesema Urassa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Siha Marathon Selina Mnkony, amesema ilianza mwaka 2019, ambapo huu ni msimu wa tano tangu kuanzishwa kwake, ikiwa na malengo makubwa ya kudumisha afya za wananchi na kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu (TB)




















