Zuberi Kidumo: Akabidhi vifaa kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya msingi Mwereni

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Injinia Zuberi Abdallah Kidumo, akiwakabidhi baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wanaosoma katika shule ya Msingi Mwereni iliyopo Manispaa ya Moshi, ikiwa ni baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Serikali.

MOSHI-KILIMANJARO.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Injinia Zuberi Abdallah Kidumo, amekabidhi vifaa saidizi katika shule ya msingi Mwereni yenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu, ikiwa ni moja kati ya shule saba zilizoko ndani ya Manispaa hiyo zinazotarajiwa kupata vifaa hivyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo katika shule ya Msingi Mwereni Injinia Kidumo amesema ya Manispaa hiyo, imepokea vifaa saidizi ikiwa ni sehemu ya vifaa vyenye thamani ya Sh bilioni nne  vilivyotolewa na serikali kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum nchini, kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi hao kufanya vizuri katika masomo yao.

Amesema serikali ya Awamu ya Sita, inayoongizwa na rais Samia Suluhu Hassan, ilielekeza Programya elimu bila malipo kwa lengo la kuwasaidia watoto wa Kitanzania kuweza kusoma.

Sambamba na hilo Injinia Kidumo, amesema kazi kubwa iliyofanyika ni suala zima la ujenzi wa miundombinu wezeshi kwa vijana wote waweze kuapata elimu.

"Sera yetu ya mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 linasema kwanza tusimuache mtoto nyumbani, kila mtoto apate elimu, inazungumzia pia suala la elimu jumuishi ambayo ni pamoja na kuhusisha wadau mbalimbali kwenye kutoa hiyo elimu". Amesema Injinia Kidumo.

Aidha amesema pamoja na Serikali kutoa elimu bila malipo pia imekuwa ikisaidia katika utekelezaji wa elimu nchini, kwa kuwasaidia watoto masikini kuweza kupata elimu hiyo.

“Sambamba na hilo Serikali imeendelea kulifanyia kazi sauala zima la ujenzi wa miundombinu wezeshi  kwa kuwawezesha walimu kuweza kufundisha katika mazingira rafiki, lakini pia na wanafunzi kuweza kusoma katika mazingira wezeshi,”. 

Akizungumzia vifaa hivyo Mstahiki Meya Zuberi Abdallah Kidumo, amesema  vifaa vilivyoletwa na serikali pamoja na pamoja na miwani, kofia, mafuta kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (albino), fimbo nyeupe, vinasa sauti (Voice Recorder), Brail pepa, Lensi kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu, komputa na vingine vingi.



 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.