Wenyeviti wa mitaa watakiwa kutatua changamoto za wananchi

MOSHI-KILIMANJARO

Chama cha Mapinduzi (CCM) Moshi Mjini kimesema kuwa, kura walizozipata Wenyeviti wa Serikali za Mtaa ni ishara ya kuaminiwa na Wananchi na kuwataka Wenyeviti hao kwenda kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.

Faraji Swai, ameyasema hayo Novemba 28,2024 alipokuwa akizungumza na viongozi hao kabla ya kuapishwa kwao, zoezi ambalo lililofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhiriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani na wananchi waliofika kushuhudia kuapishwa kwao.

Swai;  amesema wananchi wanamatarajio makubwa kwao  kuona mabadiliko halisi kupitia uongozi wao  na kwamba wenyeviti hao wanahitaji kuonyesha ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Moshi Mjini Frida Kaaya, amewataka wenyeviti hao kutenda haki na kuonyesha uongozi bora  kwa wale wanaowaongoza.

Aidha amewataka viongozi hao kuhakikisha kwamba wanakwenda kuzingatia haki, uwazi na uwajibikaji katika utendaji kazi wao wa majukumu yao, ili kuleta maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi.

“Wenyeviti wa Serikali za Mtaa na Kamati zenu mtakaokwenda kula kiapo chenu cha utalii muda mfupi ujao, nendeni mkayatekeleze yote ambao chama na serikali kimewatuma, nawaombeni sana nendeni mkafanye kazi kama timu,”amesema Kaaya.

Ameongeza kuwa “Tumemaliza uchaguzi wa serikali za mitaa jana na leo hii tunakwenda kuanza  kazi ya kuwatafutia kura za madiwani, wabunge wanaotokana na CCM pammoja na kura za  Rais Samia Suluhu Hassan,”amesema Kaaya.

Akizungumza kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Injinia Zuberi Abdallah Kidumo, Naibu Meya Stuwart Nathael, amewapongeza viongozi wote waliochaguliwa huku akiwaomba kuzingatia kanuni za utawa bora.

Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo, amesema kuwa wenyeviti hao wamebeba dhamana kubwa kwa wananchi kwenye mitaa yao na dhamana hiyo ni ya kuwatumikia wananchi.

Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Soweto Paulo Maille, amesema kuwa walifanya kampeni za kistaarabu na kufanikiwa kushinda mitaa yote mitatu, huku matarajio yake ni kuona wenyeviti walioshinda wanakwenda kutimiza ahadi zao walizoziadi  kwa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kuapishwa, baadhi ya wenyeviti akiwemo mwenyekiti wa mtaa wa kati Mussa Selemani Kitikui, mjumbe wa serikali mtaa wa vijana Benjamin Mbisye na  Musa Kitandu mtaa wa Kitandu, kwa pamoja wameahidi kwenda kuzitimisha ahadi ambazo waliziahidi mbele ya wananchi wakati wa kameni za uchaguzi serikali za mitaa amnbazo zilihitimishwa Novemba 26 mwaka huu.











Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.