Wawauvita kuwainua Wajasiriamali Moshi Vijijini

MOSHI-KILIMANJARO

Taasisi ya Wanawake na Wanaume wa Uchumi wa Viwanda Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro (WAWAUVITA) wameandaa kongamano kubwa la Wajasiriamali wadogo, litakalofanyika Novemba 30,2024 Kata ya Uru Kusini na kuhudhuuriwa na wajasiriamali takribani 250.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo Mkoa wa Kilimanjaro,  Mariam Mohamed Muhandeni,  ameyasema hayo Novemba 29,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi kuelekea kongamao hilo ambapo amesema mgeni rasmi katika kongamano hilo atakuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kilimanjaro, Shally Raymond.

Amesema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wajasiriamali wadogo, kutengeneza vikundi vitakavyowasaidia kuweza kupata mikopo ili waweze kujiinua kiuchumi na kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla.

Amesema katika kongamano hilo elimu mbalimbali zitatolewa na wataalam kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Benki ya Azania Bank, Shirika la Viwango Tanzania TBS, pamoja na wataalam kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).

Kwa upande wake Mweka Hazina wa taaisi hiyo  Magreth John amesema wajasiriamali wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo zile za ufungashaji, upatinaji wa namba ya uborana  utunzaji fedha, kupitia kongamano hilo wazalishaji hao watapata fursa kwao ya kuweza kukutana na wataalam hao wakiwemo wa TBS  na kuweza kupata utaratibu wa namna ya kupata uthibitisho wa bidhaa zao.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Wanaume wa Uchumi wa Viwanda Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro (WAWAUVITA) Mariam Mohamed Muhandeni.

Mweka Hazina wa Taasisi ya Wanawake na Wanaume wa Uchumi wa Viwanda Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro (WAWAUVITA) Magreth Jiohn


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.