MNEC Rabia; awatahadharisha Wana CCM Kilimanjaro

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Rabia Abdallah Hamid, akiwahutubia Wananchi na Wana-CCM Mkoa wa Kilimanjaro, wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika viwanja vya Pasua kata ya Bomambuzi Manispaa ya Moshi.

MOSHI-KILIMANJARO

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Rabia Abdallah Hamid, amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Kilimanjaro, kutokudharau uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kwa kusema kwamba watashinda kwa kishindo.

Hayo ameyasema Novemba 20,2024, wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya CCM ngazi ya mkoa uliofanyika viwanja vya  Pasua, Kata ya Bomambuzi , Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani humo.

Rabia ambaye pi ni mlezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, amewataka wana CCM kujitokeza kwa wingi kuwapiga kura wagombea wa CCM ili kukiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

“Uchaguzi za Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji ni muhimu sana kuliko chaguzi zozote, kwani ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi, maana viongozi wa Serikali za Mitaa ndiyo waliokaribu na wananchi hivyo ni rahisi kujua mahitaji ya kimaendeleo ili yashughulikiwe na viongozi walioko kaytika ngazi ya chini”, alisema.

Amesema “Ushindi wa CCM katika uchaguzi huu utakuwa ni msingi utakaokiwezesha kushinda uchaguzi mkuu mwakaniwa Madiwani, Wabunge na Rais”, amesema.

Aidha ameendelea kusema kuwa CCM ni chama ambacho ni tumaini kuwa kwa wananchi kutokana na uzoefu wake wa miaka mingi tangu kupigania Uhuru wa nchi na hadi kufikia maendeleo ambayo Taifa na wananchi wake wamepata tangu Uhuru.

“CCM imekuwa kinara kwenye chaguzi zote za serikali ya mitaa na uchaguzi mkuu kutokana na serikali zake zote kuhudumia wananchi vyema ikiwemo ile ya kuwasogozea wananchi huduma zote muhimu.”

Akiongea katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro,Patrick Boisafi, amesema kuwa chama hicho tawala kimesimamisha wagombea kwenye vijiji vyote 519 vilivyoko mkoani humo.

“Nitoe kwa wito kwa wapiga kura kujitokeza kwa wingi ili wagombea wa CCM waweze kuchaguliwa kwa lengo la kuendelea na kazi ya kuwahudumia wananchi”, amesema Boisafi.

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan, tayari serikali imeshaleta jumla ya Sh bilioni 915 kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika vijiji vyote mkaoni Kilimanjaro.

Akizungumza kwa niaba ya wagombea wa nafasi ya mwenyekiti mtaa wa Majengo Mapya kata ya Pasua Beatrice Kimambo ametoa wito kwa wananchi kumpa ridhaa ya kuongoza mtaa huo ili aweze kushirikiana nao katika shughuli za maendeleo katika mtaa huo.

“Katika kipindi kilichopita nlishirikiana na wananchi wa eneo hili katika shughuli za maendeleo na matokeo chanya yameonekana, ni matumaini yangu watanipa ridhaa tena ili kuendeleza pale tulipoachia kupisha uchaguzi wa mwaka huu”, amesema.

Naye mgombea wa mtaa wa Kaloleni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Ndama wa Ndama,  amesema kuwa sera za CCM zinalenga maendeleo na kwamba hayo yamedhihirika kwa maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.






 

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.