Huduma za kijamii, kiuchumi zimeimarika miaka 63 ya Tanganyika

MOSHI-KILIMANJARO.

Katika kuelekea kipindi cha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika, Tanzania inatajwa kupata mafanikio kupitia sekta ya miundombinu na huduma za kijamii.

Hayo yalibainishwa na aliewahi kuwa mkuu wa wilaya Injinia Raymond Mushi, wakati akizungumza katika mahojiano maalumu kuelekea miaka 63 ya Uhuru, ambapo amesema upatikanaji wa huduma za kijamii kama afya, elimu, maji, pamoja na ujenzi wa barabara umeimarika.

Amesema juhudi zilizofanywa na serikali zimeleta Mapinduzi katika nyanja ya afya ikiwemo kupunguza vifo virtokanavyo na uzazi na upatikanaji wa huduma bora za afya katika jamii.

Aidha, amesema mafanikio mengine yaliyopatikana katika kipindi cha kuelekea miaka 63 ya Uhuru ni pamoja na serikali kuimarisha miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege na bandari.

Ameongeza kuwa serikali imeendelea pia kuimarisha miundombinu ya elimu kwa lengo la kuhakikisha watoto wanapata elimu katika mazingira bora na yenye staha.

Kwenye sekta ya maji Mushi, amesema huduma hiyo imeongezeka kwani kabla ya Uhuru, watu wengi walikuwa wakitumia maji ya mifereji na mabwawa ambapo walikuwa wakichangia na mifugo.

Aidha amesema moja ya kazi iliyofanyika baada ya Uhuru ni kuhakikisha Tanzania inajengwa kuwa nchi moja ya Kiswahili ambayo inatumika kuwaunganisha wananchi.

“Tanzania ni mojawapo ya mataifa machache ya Afrika ambayo yanaunganishwa na lugha ya moja isiyo ya kigeni, hii ndiyo lugha isiyo na kabila, dini ukanda wala kipato, ambapo watanzanaia karibu na makundi yote wanazungunmza lugha moja ya Kiswahili.

Amesema nchi isingekuwa na jitihada za makusudi kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya taifa huenda kungekuwa na matatizo mengine ambayo yanazikuta nchi nyingine.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.