Wakulima katika kijiji cha mandaka mnono wilaya ya moshi wamlalamikia mkandarasi kufunga mfereji unaopeleka maji kwenye mashamba yao

MOSHI-KILIMANJARO.

Wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Mandaka Mnono Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, wamemlalamikia mkandarasi Ml Classic Limited JV Gilco (2000) Company Limited, kwa kufunga mfereji wa maji unaopeleka maji kwa ajili ya umwagiliaji kwenye mashamba ya kitongoji cha uswahilini na hivyo kuhofia mazao yao kukauka.

Akizungumza mkulima wa kijiji hicho Ally Mamu, anayejishughulisha na kilimoa cha mpunga amesema wameshangazwa na kitendo cha mkandarasi huyo kufika na kufukia mfereji huo licha ya kwamba tayari walikwisha kumwaga mbegu huku mahindi yakihitaji maji kwa ajili ya kunyeshea.

Amesema mkandarasi huyo, amekuja kufukia mfereji pasipo kutoa taarifa zozote, wakati tayari walikuwa wamemwaga mbegu huku mahindi ambayo walikuwa wameotesha yakihitaji maji yanakwenda kukayuka.

Wakulima wengine waliozungumzia kero hiyo ni pamoja na Esther Mshanga, Pili Yahaya, John Kitali, Joel Mchome, na Monica Mushi, wamesema kitendo cha  mkandarasi kuja na kufukia mfereji huo kinarudisha nyuma jitihada za serikali ambazo zinahamasisha wananchi kujikita katika sekta ya kilimo na kwamba wao ndio tunategemea kilimo hicho ili waweze kuuza na kurejesha mikopo ambayo wamekopo halmashauri,  kulipia ada watoto pamoja na kupata chakula.

Naye mkazi mwingine wa kijiji cha mandaka mnono Raymond Tarimo, amesena mradi huo uliletwa na serikali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi katika kilimo cha umwagiliaji, lakini cha kushangaza leo hii mradi huu, umegeuka kuwa uadui kati ya wananchi na serikali, jambo ambalo halikuwa patano hilo.

Akijibu malalamiko ya wakulima hayo Meneja wa Tume ya Umwagiliaji Mkoa wa Kilimanjaro Injinia Jacob Towa, amesema kuwa mradi wa Mandaka mnono, ulioanza muda mrefu, ulikuwa unatumika kwa njia ya asili  na mwaka 2000 hadi 2010  mfereji huo iliufanyia usanifu umbali wa mita 650, ambapo maeneo mengingine  yalibakia kuwa mfereji wa kawaida ukiwa haujasakafiwa.

Amesema mkandarasi alipata mkataba wa Sh bilioni 5.01,  ambapo kazi anazozitafanya ni pamoja na ujenzi wa mifereji yenye urefu wa mita 4500,  ujenzi wa mfereji wa kati mita wenye urefu wa mita 3650, kujenga tuta la kuzuia mafuriko kwa mto rau wenye mita 2,000, ujenzi wa mifereji ya kutoa maji mashambani yenye urefu wa kilometa mbili hadi  tano  na kwamba mradi huu ni wa muda wa mwaka mmoja kuanzia Aprili 26 mwaka 2023 hadi Aprili 25, 2025 ambapo atakabidhi mradi huo.

Kuhusu malalamiko ya kufungwa kwa mfereji huo, Injia Towa amesema kuwa yako makubaliano ambayo walikaa kikao kati ya wakulima hao na kuwaeleza kwamba pindi watakapovuna mazao yao mkandarasi ataufunga mfereji huo ili afate fursa ya kujenga mfereji huo kwani hawezi kujenga wakati maji yakiwa yanapita.

Amesema  yako makubaliano ambayowaulikubaliana na wakulima hao, kwamba eneo la mwananguruwe ni  eneo ambalo ni oevu linakuwa na maji muda wote, tuliwaomba wakulima wasiendelee  kulima ili kupisha ujenzi huo, pamoja na eneo la Makarare.

Amesema  wanufaika wa kitivo cha Makarare, Mwananguruwe, Uswahilini na Saningo, kwa upande wa tambarare kwa, wao walikuwa  wamesha panda mazao yao tuliwapa muda kuanzia Aprili  hadi Oktoba 20 mwaka huu, watakapo vuna mazao yao, wasiendelea tena kulima, lakini wameendelea kukaidi na baada ya kuvuna  wakaamua tena kumwaga mbegu ili waendelea na kilimo, jambo ambalo linakwamisha mkandarasi kuendelea na ujenzi wa skimu hiyo.














Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.