MOSHI-KILIMANJARO.
Wanaume wenye miji mitatu kwenye vitongoji tofauti, wametakiwa kuchagua
kitongoji kimoja wapo watakacho kwenda kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Noemba 27, mwaka huu.
Hayo yamesema Oktoba Mosi
na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Wilayani Mwanga, mkoani
Kilimanjaro, Wakili Edwin Lusa, wakati akizungumza na Redio Kicheko Live, kuhusu maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Wakili Lusa amesema kujiandikisha kuwa
mpiga kura zaidi ya mara moja ni kosa kisheria na kuwataka wanaume wenye mji mitatu katika
vitongoji tofauti, wanatakiwa kuchagua kituo kimoja tu kwa ajili ya kwenda kujiandikisha
kupiga kura.
“Kupiga kura ni mara moja tu, wanaume wenye
miji mitatua (familia zaidi ya kitongoji kimoja) wanapaswa kuchagua kitongoji
kimoja wapo ambacho watakwenda kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki uchaguzi
huu.”amesema.
Amesema yako maneno ya
upotoshaji yameanza kutolewa na baadhi ya vyama vya siasa, kwamba mfumo wa
uandikishaji una waruhusu wanaume wenye wake watatu kujiandikisha zaidi ya mara
moja, jambo ambalo amesema si kweli na ni kosa kisheria.
Katika hatua nyinginge Msimamizi
wa uchaguzi huo amesema kuwa halmashauri ya Wilaya ya Mwanga inatarajia
kuandikisha wapiga kura 64,000, katika uchaguzi huo.
“Kwa mujibu wa Sensa ya
watu na Makazi ya mwaka 2022 watu ambao wanasifa ya kujiandikisha kwa ajili ya
kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa wenye miaka wa kuanzia miaka 18 ni watu
64,000, uandikishaji huu utaanza Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu, ambapo vituo vya
uandikishaji vitafunguliwa kuanzania saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi
mbili jioni,”amesema Wakili Lusa.
Aidha amesema vituo vya uandikishaji katika wilaya ya Mwanga viko 291 na katika vituo hivyo wananchi watapata fursa ya kujiandikisha.