SAME-KILIMANJARO
Wakazi wa Kijiji cha
Mgando, Kata ya Bendera Wilaya ya Same, wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi
wa barabara ya Ndungu-Mkomazi, yenye kilometa 36 inayojengwa kwa kwa kiwango
cha lami.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti na Waandishi wa habari waliotembelea barabara hiyo, ili kujionea ujenzi
wake wakazi hao Bony Msifuni, Michael Mbwmbo, Amir Juma na Haros Victor, wamesema
kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami, itakwenda kufungua
fursa za kiuchumi na biashara hasa kwa
wakulima wa mpunga, ndizi na tangawizi.
Aidha wamesema
kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kwa
kiwango ncha lami vijana wengi wataweza kupata fursa za ajira kupitia shughuli
za Bodaboda hivyo kuboresha maisha yao
na maendeleo ya kijiji chao.
Kwa upande wake Meneja
wa Wakala Barabara (TANROADS) MKoa wa Kilimanjaro Mhandisi Motta Kyando,
amesema ujenzi wa barabara hiyo ukikamilika utafungua uchumi wa wakazi wa
Wilaya ya Same, ambao kwa kiasi kikubwa unategemea shughuli za kilimo cha mazao
ya tangawizi, mpunga na ndizi na
kuhuisha utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mkoamazi.
Amesema barabara ya
Ndungu hadi Mkomazi, ina kipande kilometa 36.9, amesema tayari serikali kupitia
Wakala wa Barabara imesaini mkataba wa kuweza kuanza kazi ya ujenzi kwa kiwango
cha lami.
Amesema mkataba wake
ulisainiwa mwezi Januari mwaka huu, ambapo mradi huo utachukua miezi 18 ifikapo
Desemba mwaka 2025 kazi ya ujenzi
itakuwa imekamilika.
Kyando amesema barabara
hiyo endapo itakamilika itakuwa na manufaa makubwa sana, kwaniu kutakuwa na
maendeleo makubwa kwa, vijana ambao watapata ajira na kukuza uchumi baada ya watalii kuongezeka na watu wataona
urahisi wa kufika katika hifadhi ya mkomazi.
