Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Mjini na Mwenza wake Mama Mary Moshi, pamoja
na familia yake wameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura
kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika kituo cha Zahanati Kata ya
Bondeni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Akizungumza Oktoba
13,2024 mara baada ya kujiandikisha Swai amesema kuwa zoezi la kujiandikisha
katika daftari la kupiga kura ni muhimu kwa kuwa ni wajibu kushiriki katika
kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia wananchi.
Amesema viongozi wa
Serikali za Mitaa ndiyo wanaoishi jirani zaidi na wananchi hivyo ni muhimu kushiriki
katika kuwachagua wale watakaolinda maslahi ya jamii husika.
Swai ameongeza kwamba
upatikanaji wa viongozi wazuri unaanza kwa kujiandikisha katika mazoezi yote ya
uchaguzi yanayotarajiwa hivi karibuni.
Hali kadharika Swai
ametoa wito wa kipekee kwa wanawake kujitokeza katika kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi kwa kuwa wanazifahamu vema changamoto za jamii na pia
wanao uwezo wa kuongoza vizuri.
Amesisitiza wananchi
kushiriki vema chaguzi zote kwa amani na utulivu kwa kujiepusha na lugha zisizo
na staha pamoja na vurugu wakati wa kampeni.
Eva Paulo (kulia) akimsikiliza kwa makini maelekezo anayopatiwa na Mwandishi wa Daftari la Wapiga kura Bi. Agripina Raphael kabla ya kujiandikisha katika daftari hilo.
Mary Moshi akijiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini Faraji Kibaya Swai, akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mwandishi wa Daftari la Wapiga kura Bi. Agripina Raphael kabla ya kujiandikisha.






