Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Nurdin H. Babu, akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024
MOSHI-KILIMANJARO.
Jumla ya vituo 2,368, vinatarajiwa
kutumika kwa ajili ya wananchi mkoani Kilimanjro kujiandikishia kwenye Daftari
la Mkazi linalotarajiwa kuanza Oktoaba 11, mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Nurdin Babu, ameyasema hayo mnmo Oktoba 10, 2024, Wakati
akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake, ambapo amesema uandikishaji
wa wapiga kura utafanyika Oktoba 11 hadi Oktoba 20,2024 kwenye vituo vilivyopangwa.
Amesema wakazi wenye sifa za kupiga kura wenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi na wale wanaokidhi masharti ya kisheria amewahimiza kushiriki kwa wingi katika uchaguzi huo.
“Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa ni nguzo muhimu ya Kidemokrasia ya ushirikishwaji na uwajibikaji kwa jamii, ambapo kila mtu anahitajika
kushiriki kikamilifu ili wapatikane viongozi ambao ni wawajibikaji kwa
mustakabali mwema wa maendeleo ya nchi”, amesema.
Kwa mujibu wa Kanuni
ya 9 ibara ya pili ya Tanzazo la
Serikali Na. 574 linalohusu Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe
wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka za
Miji, maelekezo haya yanafafanua hatua
zitakazoongoza mchakato wa uchaguzi, kuanzia uandikishaji wa wapiga kura,
uchukuaji na urejeshaji wa fomu za
kugombea ,uteuzi wa wagombea na tarehe ya siku ya uchaguzi.
Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kusema kuwa “Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakuwa ni miongoni mwa ishara za kutekeleza misingi ya demokrasia kupitia uchaguzi huru, wazi na haki.”