MOSHI-KILIMANJARO
Mkoa wa
Kilimanjaro unatarajia kuandikisha watu milioni 1172,394 waliofikisha umri wa
miaka 18 na kuendelea, kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika
Oktoba 11, mwaka huu.
Mratibu wa
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mkoa Gasper Ijiko, ameyasema hayo mnamo Oktoba 10, 2024 wakati akizungumza na
waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusu zoezi la uandikishaji wapiga kura
litakalofanyika Oktoba 11 mwaka huu na kuhitimishwa Oktoba 20,2024.
Amesema maoteo ya
takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Wanaume wanaotarajiwa
kuandikishwa ni 559,676 wakati Wanawake ni 612,718.
“Mkoa wa
Kilimanjaro tunatarajia kuandikisha watu ambao wamefikisha umri wa miaka 18,
Wanaume wanatarajiwa kuandikishwa ni 559,676 na Wanawake ni 612, 718 ambapo maoteo
yetu ya uandikishwaji ni milioni 1172,394.”amesema Ijiko.
Aidha amesema kuwa zoezi la uandikishaji wapiga kura
linatarajiwa kuanza Oktoba 11 mwaka huu hadi Oktoba 20 ambapo jumla ya vituo
vya kujiandikishia katika mkoa huo viko 2,368 kuanzia vijiji na vitongoji.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Nurdin Babu, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kuweza
kutimiza wajibu wa kikatiba wa kuchagua na kuchaguliwa.
“Kama mnavyofahamu mwaka huu ni mwaka wa
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo tunaenda kufanya uchaguzi wa Viongozi wa
Serikali za Mitaa, utakaohusisha Wenyeviti wa Vijiji, Mitaa, Vitongoji na Wajumbe wa Serikali za Vijiji na Mitaa.”amesema.
Akizungumzia masuala la Kidemokrasia Mkuu
huyo wa mkoa amesema kuwa Tanzania ni nchi Uhuru, ambapo wananchi wake
wanapaswa kuamua kuhusiana na namna ya kuendesha masuala ya msingi kuhusiana na
serikali zao.
Babu amesema; baada ya wananchi kujiandikisha
katika daftari la Orodha ya wapiga kura, kutakuwepo na zoezi la kukagua orodha
ya wapiga kura ambapo orodha yote ya wapiga kura kuanzia kitongoji hadi mtaa
itabandikwa kenye mbao za matangazo, ili wananchi waliojiandikisha kutoa
pingamizi katika uandikishaji wa maji yao.
“Zoezi hili litafanyika kuanzia Oktoba 21
hadi Oktoba 27 mwaka huu,”alisema Babu.