Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, akijiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura Serikali za Mitaa Oktoba 12, 2024 kijijini kwake Chomvu Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, kulia kwake ni Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Mwanga Bi Zahara Msangi na Mwandishi wa Daftari la Wapiga Kura Kata ya Chomvu Mussa Abdallah Lupatu.
MWANGA-KILIMANJARO
Waziri
Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu
Cleopa Msuya, ametoa wito kwa Vyama vya Siasa Nchini, kuhakikisha kwamba wanateua wagombea wenye
uwezo na maadili katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika
Novemba 27 mwaka huu nchini kote.
Msuya
aliyasema hayo Oktoba 12,2024, muda mfupi baada ya kujiandikisha kwenye Daftari
la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu, nyumbani kwake katika kijiji cha
Chomvu Wilayani Mwanga mkoani
Kilimanjaro.
Msuya
amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kufanya kazi kwa karibu na wananchi ili
kutatua changamoto zao na kuboresha maisha yao.
“Uteuzi
mzuri wa wagombea utasaidia kuimarisha demokrasia na maendeleo katika maeneo
mbalimbali hapa nchini.”alisema Msuya.
Aliongeza
kuwa “Vyama vya Siasa nchini, ambavyo vitashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Novemba 27 mwaka huu, wahahakikishe kwamba wanateua wagombea wazuri ambao
wakibahatika kushika nafasi za uongozi watafanya kazi za wananchi kwa manufaa ya
wananchi na Taifa kwa ujumla,”amesema.
“Serikali
yoyote iliyoko madarakani msingi mkubwa ni Serikali za Mitaa; na hiki ni
kipindi muhimu kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na kutumia haki zao za
kuchagua viongozi waadilifu ambao wataongoza Serikali za Mitaa, Vijiji na
vitongoji kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.”amesema.
Kwa upande
wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Zahara Msangi, amesema kuwa zaidi
ya watu 84,000 wanatarajiwa kujiandikisha katika wilaya ya Mwanga, ambapo
katika Kata ya Chomvu zaidi ya watu 4,000 wanatarajiwa kujiandikisha.
“Nichuku
fursa hii kukushukuru wewe Waziri Mkuu Mstaafu kwa kuja kujiandikisha kwani
uamuzi wako huo utaleta hamasa kubwa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha,”amesema
Msangi.
Akizungumza
msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Wakili
Edwin Lusa, ametoa rai kwa wananchi kutumia haki zao za msingi kwa kujitokeza
kwa wingi kujiandikisha na hata kugombea nafasi zilizoko kwa mujibu wa taratibu
za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Naye Mkuu
wa Wilaya ya Mwanga mwanahamisi Munkunda, amemshukuru Waziri Mkuu Mstaafu
Cleopa Msuya, kwa kuwa mstari wa mbele na kuungana na Wananchi wa Kata
anayoishi kujitokeza kuja kujiandikisha.
Munkunda
alisema kila linapokuja jambo la kimaendeleo
katika ngazi ya Wilaya, ngazi ya Mkoa hata kwa ngazi ya Taifa Msuya
amekuwa msitari wa mbele kushiriki jambo hilo.
Awali
akiwasilisha taarifa yake Afisa mtendaji Kata ya Chomvu Omari Salim Kiangi, amesema
kuwa jumla ya watu 4,291 wanatarajiwa kujiandikisha kwenye kata hiyo, ambapo
alisema kati yao wanaume ni 1,822 na wanawake ni 2,469.
“Kwa
siku ya kwanza lililoanza zoezi hili la uandikishaji Daftari la wapiga kura
Oktoba 11, mwaka huu, mambo yalienda vizuri kwani waliandikisha jumla ya watu
991, ambapo kati yao wanaume walikuwa ni 449 na wanawake ni 522,”amesema
Kiangi.
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, akijiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura Serikali za Mitaa, kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Mwanga Bi. Mwahamisi Munkunda, na kulia kwake ni Mkurugenzi halmashauri ya Mwanga Bi Zahara Msangi
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Mwanga Bi. Zahara Msangi, Msimamizi wa Uchaguzi Serikali za Mitaa Wakili Edwin Lusa na Diwani wa Kata ya Chomvu Shaghira Mchomvu.
Msimamizi wa Uchaguzi Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mwanga Wakili Edwin Lusa, akitoa tathmini ya namna ya Wananchi wa Wilaya hiyo wanavyojitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mwanga Bi. Zahara Msangi, akitoa maelezo ya namna zoezi la uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura Serikali za Mitaa
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bi. Mwanahamisi Munkunda (kulia)akizungumzia suala la Uandikishaji wa wananchi katika Daftari la Wapiga kura Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bi. Mwanahamisi Munkunda na Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Mwanga Bi. Zahara Msangi.
Mhe; Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu Cleopa Msuya, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bi. Mwanahamisi Munkunda na Mwandishi wa Daftari la Wapiga kura Kata ya Chomvu Bw. Mussa Lupatu.
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya wa tatu kutoka kulia, akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mwanga Bi. Mwanahamisi Munkunda , Mkurugenzi wa halmashauri ya Mwanga Bi Zahara Msangi, Mwanasheria wa halmashauri Edwin Lusa na Diwani wa Kata ya chomvu Shaghira Mchomvu









