Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI)-Moshi kimeanzisha kozi fupi ya biashara ya hewa kaboni, ambayo imelenga kuifanya nchi kunufaika na zao hilo jipya la misitu.
Mkuu
wa chuo hicho Dkt. Zacharia Lupala, ameyasema hayo Oktoba 31,2024, wakati
akizungumza katika mahojiano maalumu na
Moshi FM iliyotembea chuo hicho na kutaka kufahamu mafanikio ya chuo hicho
tangu kuanzishwa kwake mwaka 1976.
Dkt. Lupala amesema chuo hicho kimeongeza kozi ya mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu, ambayo ni biashara ya hewa kaboni, kutokana na kuwa na faida nyingi ikiwamo ya kupata fedha za kigeni.
Dkt. Lupala amesema liicha ya Tanzania kuwa na utajiri wa misitu, bado fursa ya biashara ya hewa kaboni, haijatumika ipasavyo, hatua ambayo imekisukuma chuo hicho, kuanzisha kozi fupi katika sekta hiyo.
Amesema pamoja na nchi ya Tanzania kuwa na kiwango kikubwa cha hewa kaboni, bado inakabiliwa na wataalamu wenye ujuzi kuhusiana na biashara hiyo, ambapo chuo kimekuja na mpango wa kuanzisha kozi fupi inayotokana na biashara ya hewa kaboni.
Amesema Chuo cha Viwanda na Misitu FITI kina Wataalamu wabobezi wenye fani hiyo, ambao watakwenda kuwasaidia Watanzania kutengeneza kampuni za uwakala (carbon blocker), uandishi wa mawazo ya biashara ya hewa kaboni, upimaji na namna ya kufanya majadiliano ya biashara katika soko la kimataifa.
Aidhaamesema kuwa watanzania hawana budi kuchangamkia fursa za biashara ya hewa kaboni na kwamba kwa kukitumia Chuo cha Viwanda vya Misiti Moshi FITI kwa kuwaleta vijana wao katika chuo hicho watapata mafunzo hayo.
Asilimia
55 ya ardhi ya Tanzania inatajwa kuwa ni hifadhi za misitu, hivyo kuwa na fursa
kubwa ya biashara ya hewa kaboni kwenye soko la Kimataifa watanzania watakwenda
kunufaika na fursa ya biashara hiyo yenye mtazamo wa kuhifadhi mazingira.