MOSHI-KILIMANJARO.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 27 ya Chuo cha Viwanda na Misiti-Moshi (FITI) yatakayofanyika Novemba Mosi mwaka huu chuoni hapo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Oktoba 30, 2024 Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi na Mkuu wa Kitengo cha mahusiano katika Chuo hicho Cesilia Lyimo, amesema kuwa wahitimi 340 wanatarajiwa kuhitimu masomo yao kwa mwaka wa masomo 2023/ 2024.
Bi. Cesilia Lyimo, amesema kuwa chuo hicho kinajivunia mafanikio mengi, ikiwemo kuendelea kufanya kazi na kutoa mafunzo ya kiufundi na kitaaluma katika Sekta ya Misitu, huku kikijitahidi kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kuboresha ujuzi wa wafanyakazi tangu kuanzishwa kwake mwaka 1976.
“Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) ni Taasisi ya umma inayofanya kazi chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ambapo FITI ilianzishwa Novemba mwaka 1976 kwa msaada wa kifedha kutoka Serikali ya Sweden.”amesema
Ameongeza kuwa Mwanzoni, lengo kuu la taasisi hiyo ilikuwa kuwaelekeza Wafanyakazi wa kati wanaohitajika katika uendeshaji wa Sekta ya miti inayomilikiwa na Serikali, inayojulikana kama Tanzania Wood Industries Corporation (TWICO) na Mwishoni mwa kipindi cha ufadhili wa Sweden mwaka 1980, FITI ilifanikiwa kupata msaada wa kifedha kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Finland (FINNIDA) kwa kipindi cha mwaka 1980 hadi 1988.
Amesema kuanzia mwaka 1988 hadi sasa, FITI inaendeshwa na Serikali ya Tanzania na lengo lake kuu ni kutoa mafunzo maalum ya kiufundi katika Sekta ya Misitu na huduma katika Sekta ya Miti.
Ameongeza kuwa “Hadi sasa FITI imeendelea kuzalisha wahitimu
wengi katika ngazi za Astashahada na Stashada.Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi (FITI) Bi. Cesilia Lyimo, akizungumza na Waandishi wa habari hawapo katika picha, kuhusiana na maandalizi ya mahafi 27 ya chuo hicho yatayofanyika Novemba 1, 2024.