MOSHI-KILIMANJARO
Chuo cha Viwanda vya
Misiti (FITI) kilichoko Moshi, mkoani Kilimanjaro kimeendelea kuboresha mitaala
ya chuo hicho, lengo likiwa ni kuhakikisha mbali na kupata ajira, pia wahitimu
wa chuo hicho waweze kujiajiri wenyewe.
Hayo yameelezwa Oktoba
30,2024 na Mkuu wa chuo hicho Dkt. Zakaria Lupala wakati akizungumzia mafanikio
ya chuo hicho kuelekea mahafali ya 27 yanayotarajiwa kufanyika mwezi Novemba
Mosi, mwaka huu.
“Chuo hiki kinatoa
mafunzo ya aina mbalimali yakiwemo yale ya matumizi bora ya bidhaa za misitu na
uhifadhi wa mazingira; mitaala yake pia inaboreshwa ili wanafunzi waweze kupata
ujuzi utakaowawezesha kujiajiri’, alisema.
Ameendelea kusema
“Mitaala yetu inalenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa kuhifadhi raslimali za Taifa,
kuwa wabunifu kupitia uchakataji wa bidhaa za misitu kwa kutumia teknolojia ya
kisasa na pia kuwa wafanyabiashara wazuri wa mazao yanayotokana na misitu,” amesema.
Amesema mbali na
kupata ajira, mwanafunzi anayehitimu Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi (FITI)
anakuwa tayari amepata ujuzi wa aina mbalimbali kama vile ufundi seremala na
hivyo kuweza kujiajiri yeye mwenyewe kwa kufungua karakana yake mwenyewe badala
ya kusubiri kuajiriwa.
Dkt. Lupalo kusema
kuwa wanafunzi wa chuo hicho hupata elimu ya ufundi kwa vitendo zaidi, ambapo
alisema kuwa pia wanapata elimu ya uzalishaji mali, ile ya upandaji na
uvunaji wa miti.
Aidha amesema kuwa
wanafunzi hao wanapta nafasi ya kushiriki kwa vitendo usimamizi na uhifadhi
misitu, kwenye taasisi mbalimbali zikiwemo zile zilizo chini ya Wizara ya
Maliasili na Utalii kama vile Ngorongoro, Tanapa, Tawa pamoja na taasisi
binafsi.
Kwa upande wake Afisa
mahusiano wa Chuo hicho Cesilia Lyimo, amesema chuo hicho kinatarajia kufanya
mahafali yake ya 27 ambayo yanatarajiwa kufanyika chuoni hapo Novemba 1,
mwaka huu, huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu (Maliasili) Wizara ya
Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas.
Amesema katika
mahafali hayo jumla ya wanafunzi 340 wanatarjiwa kuhitimu katika mahafali hayo
baada ya kupata mafunzo chuoni hapa kwa muda wa masomo waliokuwa wamepangiwa.Mkuu wa Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi (FITI) Dkt. Zacharia Lupala, akizngumzia mafanikio ya chuo hicho toka kuanzishwa kwake mwaka 1976.
Muonekano wa jengo la Utawala katika Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi FITI